Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Alain Juppé atuhumiwa kukigawa chama cha mrengo wa kulia

Katika makala iliyochapishwa Alhamisi hii, Novemba 24 katika gazeti la Le Figaro, wabunge wengi wa chama cha mrengo wa kulia wametoa wito kwa utulivu baada ya Alain Juppé kumshambulia kwa maeneno makali François Fillon.

Alain Juppé, Meya wa mji wa Bordeaux na mgombea wa sasa katika kura za mchujo, Novemba 20, 2016.
Alain Juppé, Meya wa mji wa Bordeaux na mgombea wa sasa katika kura za mchujo, Novemba 20, 2016. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Alain Juppé, Meya wa mji wa Bordeaux ambaye alishindwa kwa alama 15 dhidi ya mshindani wake François Fillon katika duru ya kwanza ya kura za mchujo Jumapili iliyopita, alikashifu msimamo wa mshindani wake kuhusu utoaji mimba, na kufuta baadhi ya idara katika sekta ya uuma. Wengi wamemtuhumu kwamba ana lengo la kusambaratisha chama cha mrngo wa kulia

Katika makala haya ya Le Figaro, Wabunge na Maseneta 215 wamesikika wakisema"pamoja, tujadili hali hii." Wawakilishi hawa wanalaani "kashfa" za Alain Juppe dhidi ya François Fillon, wakati ambapo tangu kutangazwa kwa matokeo ya duru ya kwanza ya kura za mchujo, Meya wa mji wa Bordeaux hakusita kumuaibisha mpinzani wake katika kura za msingi. Wawakilishi hao kutoka chama cha mrengo wa kulia wametoa wito wa kuheshimiana katika mjadala.

Jumatano wiki hii wabunge wengi wa Bunge la Ufaransa walitoa wito wa kumkanya Alain Juppé.

Wawili hao waliopata ushindi katika duru ya kwanza ya kura za mchujo watapambana Alhamisi hii usiku katika mjadala wa mwisho kwenye televisheni. Kwa mujibu wa utafiti wa Ifop kwa niaba ya Paris Match, iTELE na Sud Radio, François Fillon atashinda kwa 65% ya kura katika duru ya pili ya kura za mchujo Jumapili ijayo, dhidi ya 35% ya kura atakazopata Alain Juppé.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.