Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Siasa - Uchumi

Barack Obama awasihi Wamarekani kuhusu Donald Trump

media Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani ya White House, Novemba 14, 2016. REUTERS/Yuri Gripas

Jumatatu hii Novemba 14 Barack Obama amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu kufanyika kwa uchaguzi wa urais ambapo Donald Trump aliibuka mshindi. Rais Obama ambaye anayemaliza muda wake amewataka Wamarekani kukubali matokeo ya uchaguzi, bila hata hivyo kumpinga mrithi wake.

Mkutano huu na waandishi wa habari ulionekana kama ni katika hatua ya kwanza ya kuaga, ambamo Obama anaendelea kushilikilia madaraka hadi Januari 20. "Raia wameamua, Donald Trump atakuwa rais atakaye nirithi, rais wa 45 wa Marekani, alisema rais wa Marekani ambaye alifanya kampeni dhidi ya Donald Trump. Na wale ambao hawakumpigia kura wanapaswa kutambua kuwa hivyo ndivyo demokrasia ilivyo, ni mfumo wetu. Nadhani ni muhimu kumuacha achukuwe maamuzi, na raia wa Marekani wataona, kwa kipindi cha miaka miwili ijayo kama wanapenda kile wanachoona, kama ni aina ya sera na mwelekeo kwa ajili ya nchi ambavyo walikua wanatarajia. Nilimwambia, na nayarejelea hadharani, kwamba kwa sababu ya mazingira ya kampeni hii, hasira, maneneo ya chuki, ni muhimu sana kwake kuonyesha ishara ya umoja kwa kufikia watu wachache ambao wamehisi kulengwa na hotuba alizokua akitoa wakati wa kampeni, " amesema Rais Barack Obama.

Rais Barack Obama amewahakikishia washirika wa Marekani kwamba Donald Trump ataendeleza heshima na ushirikiano wa kimataifa baina ya nchi yake nao wakati yeye atakapokabidhi urais mwezi Januari. Rais Obama amesema kwamba Donald Trump ameonesha nia ya kutaka kudumisha uhusiano baina ya Marekani na muungano wa kujihamia wa nchi za Magahribi (NATO).

Obama amesema kwamba Marekani lazima iendelee kuwa nguzo ya nguvu na ya matumaini kwa watu duniani kote. Na kuongeza kusema kwamba uhusiano baina ya nchi na nchi unakwenda mbali zaidi ya nafasi ya urais na wanadiplomasia,majeshi na kwamba wakuu wenye hekima na busara wataendelea kuonesha ushirikiano na wenzao wanaoshughulikia masuala ya kigeni.

NATO yamuonya Trump kuhusu uamuzi dhidi yake

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltennburg amemuonya rais mteule wa Marekani Donald Trump dhidi ya kufanya maamuzi ya kipekee, akisema kuwa sio chaguo la muungano wa Ulaya ama hata Marekani.

Amesema kuwa mataifa ya magharibi yalikabiliwa na changomoto yake kuu ya kiusalama.

Wakati wa kampeni zake za uchaguzi bwana Trump aliutaja muungano huo wa kijeshi wa mataifa ya Magahribi kama uliopitwa na wakati.

Alisema kuwa Marekani itafikiri mara mbili kumsaidia mwanachama yeyote wa muungano huo ambaye ameshambuliwa iwapo hajalipa kodi yake ya uanachama.

Akiandika katika gazeti moja la Uingereza Observer,bw, Stoltenberg alikiri kuhusu umuhimu wa baadhi ya wanachama kulipa kodi ya juu kwa kuwa Marekani inagharamikia asilimia 70 ya matumizi ya muungano huo.

Lakini ameongezea kuwa viongozi wa Marekani wamekuwa wakitambua kwamba wana washirika muhimu barani Ulaya kupitia usalama na udhabiti walio nao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana