Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA

Donald Trump awateua kwenye nafasi muhimu watu wake wa karibu

Rais mteule Donald Trump amewateua Jumapili hii Novemba 13 watu wawili muhimu miongoni mwa watetezi wa ushindi wake kwenye nyadhifa muhimu. Reince Priebus, mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya chama cha Republican, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu ya White House, na Steve Bannon ameteuliwa kuwa Mshauri Mwandamizi na Mkuu wa Mipango.

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump.
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi wa Reince Priebus uongozi wa utawala wa Trump na Steve Bannon kama Mkuu wa Mipango umepokelewa kwa furaha na wasiwasi.

■ Reince Priebus, mpatanishi

Reince Priebus, hapa kwenye kusanyiko la Chama cha Republican katika Cleveland, Julai 17, 2016.
Reince Priebus, hapa kwenye kusanyiko la Chama cha Republican katika Cleveland, Julai 17, 2016. REUTERS/Mike Segar

Uteuzi wake kama Katibu Mkuu Ikulu ya White House umepokelewa kwa furaha. Hakuna mtu anayepinga kwa kweli uteuzi wa Reince Priebus ambaye atasimamia mambo yote ya Ikulu hasa upande wa wafanyakazi kwa kuhakikisha kuimarika kwa utawala wa chama cha Republican. Licha ya kukosolewa na baadhi ya wafuasi wa chama cha Republican wanaompinga Donald Trump, Reince Priebus alikataa kuachana na Donald Trump, hasa baada ya kutawazwa katika mkataba wa chama cha Republican. Pia alifanya kazi kwa bidii kwa kuwahamasisha wale ambao walikua wampendi Donald Trump kuungana pamoja naye katika dakika za mwisho.

Priebus pia ni rafiki wa Spika wa Baraza la Wawakilishi, Paul Ryan. Katibu Mkuu wa Ikulu ya White House anaweza kumsaidia Trump ili kuwezesha uhusiano wake na Congress.

■ Steve Bannon, mtu anayetia wasiwasi

Steve Bannon, hapa katika mkutano wa hadhara mjini New York Agosti 20, 2016.
Steve Bannon, hapa katika mkutano wa hadhara mjini New York Agosti 20, 2016. REUTERS/Carlo Allegri

Kwa upande mwengine, uteuzi wa Steve Bannon kama Mkuu wa Mipango, unatia wasiwasi. Alikua Mwenyekiti wa Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia, ambayo imekua ikirusha taarifa za ubaguzi wa rangi, fitina na ubaguzi kwa Waislamu, kwa manufaa ya Wamarekani Wazungu.

Donald Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.