Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-UHAMIAJI

Trump ataka kufukuza hadi wahamiaji haramu milioni 3 nchini Marekani

Rais mpya wa Marekani aliyechaguliwa Donald Trump anataka kufukuza hadi wahamiaji haramu milioni 3 nchini humo. Amethibitisha haya katika sehemu ya mahojiano yaliyorushwa Jumapili hii jioni kwenye televisheni ya CBS, ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa rais wa Marekani. Mahojiano haya yalifanyika Ijumaa Oktoba 11.

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, na mkewe Melania katika mji wa Manhattan.
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, na mkewe Melania katika mji wa Manhattan. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Tutakachofanya ni kuchukua watu ambao ni wahalifu na ambao wana rekodi ya uhalifu, ambao ni kutoka katika makundi majambazi, ambao ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, bila shaka wanakadiriwa takribani milioni 2, inawezekana pia wakafikia watu 3 milioni, tutawafukuza hapa nchini au tuwaweke katika jela. Lakini tunapaswa tu kuwafukuza kutoka nchini mwetu, wanaishi hapa kinyume cha sheria, " amesema Donald Trump.

Kituo cha CBS kilianza kurusha sehemu ya mahojiano hayo kwenye tovuti yake, sehemu ya mazungumzo kuhusu uhamiaji.

Rais mteule amepunguza ahadi aliyoitoa kwa muda mrefu wakati wa kampeni yake. Kwanza aliahidi kufukuza jumla ya wahamiaji haramu milioni 11 waishio nchini Marekani, wakati mwingine kwa miongo kadhaa. Mwishoni mwa mwezi Agosti, baada ya muda mrefu akisita sita, alirejelea ahadi hiyo akibaini kwamba anataka tu kufukuza watu 'wabaya', akimaanisha wahalifu.

Donald Trump pia amezungumzia juu ya moja ya miradi yake kabambe katika utawala wake, ambayo ni ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico. Alipoulizwa mwandishi: "Wewe unategemea kweli kujenga ukuta kwenye mpaka na Mexico? " Rais wa 45 wa Marekani amejibu "ndiyo", lakini ameeleza kuwa ukuta huo unaweza kweli kuwa sehemu ya ukuta na "baadhi ua. " "Katika baadhi ya maeneo, napenda kujengwe ua, kwingineko, ukuta ni sahihi," amesema, huku akiongeza kwa sauti ya ucheshi: "Mimi napenda sana kuhusu ujenzi. "

Donald Trump pia amezungumzia juu ya moja ya miradi yake kabambe katika utawala wake, ambayo ni ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.
Donald Trump pia amezungumzia juu ya moja ya miradi yake kabambe katika utawala wake, ambayo ni ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico. Michael Vadon/ pixabay

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.