Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SAIASA

Uchaguzi Marekani: wagombea waendelea kuwasaka wapiga kura

Donald Trump amekua akiendelea kwa kasi na kampeni zake siku ya Jumapili Novemba 6, ikiwa imesalia siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais wa Marekani, wakati ambapo Hillary Clinton amekua akiendelea na kampeni zake katika ngome kuu za chama cha Democratic ambazo haitaki kupoteza.

Donald Trump na Hillary Clinton wakati wa mjadala wao wa kwanza Septemba 26, 2016.
Donald Trump na Hillary Clinton wakati wa mjadala wao wa kwanza Septemba 26, 2016. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Mbio hizi za kuwania mamlaka ya uongozi wa nchi ya Marekani ni za mwisho, kwani bado zimesalia siku zisizozidi mbili kabla ya uchguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwanzoni mwa wiki hii.

Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump ameendelea kujikusanyia wapiga kura wengi katika siku za hivi karibuni, kwa mujibu wa utafiti unaoendelea.

Donald Trump yuko katika nafasi ya kutafuta idadi kubwa ya wapiga kura kwa lengo la kumuangusha mshindani wake kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton, ambaye hata hivyo bado anaongoza katika kinyang'anyiro hiki, kwa mujibu wa utafiti unaoendelea.

Ndani ya masaa 48 kabla ya uchaguzi huu, ulimwengu mzima umeelekeza macho yake nchini Marekani, ukijiuliza iwapo nchi ya kwanza yenye nguvu duniani itaongozwa na rais mwanamke ambapo itakua mara ya kwanza katika historia ya taifa hili, au mtu itaongozwa na mtu anayekosoa tawala za marais wa chama cha Democratic, ambaye anataka kufanya mabadiliko katika utawala wa Washington.

Utafiti wa hivi karibuni wa vituo vya NBC / Wall Street Journal unasema Hillary Clinton anaongoza kwa 44% za kura dhidi ya 40%alizo nazo mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika ngazi ya taifa. Hata hivyo wagombea hao bado wanakaribiana sana.

Runinga ya CBS siku ya Jumapili Novemba 6, ilibani kwamba wagombea wote wawili walikua wakikaribiana katika majimbo ya Ohio na Florida.

Hata hivyo wachambuzi wa uchaguzi wa Marekani wanabaini kwamba Bi> Clinton atashinda kura mbili dhidi ya moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.