Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-UCHAGUZI

Trump: tayari uchaguzi kugubikwa na wizi wa kura

Wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amesema akisisitiza kwamba tayari kugubikwa na wizi wa kura uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Novemba kwa ushindi wa mshindani wake kutoka chama cha Democrat Hillary Clinton. Kambi ya Bw Trump imezingatia kwa makini matamshi hayo.

Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump akiomba radhi kwa taarifa aliyotoa kisha  kwa video iliyorushwa hewani,Oktoba 8, 2016.
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump akiomba radhi kwa taarifa aliyotoa kisha kwa video iliyorushwa hewani,Oktoba 8, 2016. Reuters/Handout
Matangazo ya kibiashara

"Kura zinakaribiana lakini mnaweza kuamini kuwa nimepoteza idadi kubwa ya wapiga kura kwa misingi ya matukio ambayo kamwe hayakutokea. Vyombo vya habari vinachangia kwa wizi wa kura katika uchaguzi huu!", Donald Trump amesema Jumapili hii asubuhi kwenye Twitter. Bilionea huyu anashtumiwa na wanawake kadhaa kwa kuwashambulia au kuwayanyasa kimapenzi bila idhni yao.

Wakati ambapo wanasiasa wengi, upande wa chama cha Democrat sawa na upande wachama cha Republican, wana wasiwasi kuhusu uwezekano wa madhara kufuatia kauli ya Donald Trump, ambaye alikua akitoa mbele ya umati wa watu, mgombea mwenza Mike Pence amekua akituliza hali hiyo ya sintofahamu iliyoibuka katika chama cha Republican baada ya shutma dhidi ya Donald Trump.

"Kwa kweli tutakubali matokeo ya uchaguzi," amesema Bw Pence katika makala ya "Meet the Press" ya runinga ya NBC, akikumbusha kwamba Donald Trump aliahidi hivyo wakati wa mjadala wa kwanza.

"Tutapambana hadi Novemba 8 na bila shaka tutakubali uamuzi wa wananchi wa Marekani," Mike Pence ameongeza.

Uchunguzi wa mwisho katika ngazi ya kitaifa uliyoendeshwa na NBC / WSJ na kutolewa Jumapili hii asubuhi, unaonyesha kuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton anaongoza kwa alama 11 dhidi ya Donald Trump (sawa na 48% dhidi ya 37%). Uchunguzi mwingine, uliyoendeshwa na ABC / Washington Post, unaonyesha kuwa Hillary clinton anaongoza kwa alama 4 didi ya mshindani wake Donald Trump (sawa na 47% dhidi ya 43%).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.