Pata taarifa kuu
MAREKANI-DONALD TRUMP

Wanawake 2 wamshtumu Donald Trump kuwapapasa kimapenzi

Gazeti la New York Times limechapishwa Alhamisi hii asubuhi ushahidi wa wanawake wawili ambao wanasema kuwa walishambuliwa kingono na Donald Trump. Mgombea urais wa chama cha Republican tayari ameumbuka na video ya mwaka 2005 ambapo anazungumzia mambo ya uasherati.

Donald Trump, akiwa na bango mkononi lililoandikwa "wanawake pamoja na Trump", katika mkutano wa hadhara mjini Lakeland, Oktoba 12, 2016.
Donald Trump, akiwa na bango mkononi lililoandikwa "wanawake pamoja na Trump", katika mkutano wa hadhara mjini Lakeland, Oktoba 12, 2016. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Watu wengi nchini Marekani wanajiuliza kwa nini Donald Trump hakusikia ushauri mwema kutoka kwa wajumbe wa chama cha Republican kwa ajili yake, wale waliomshauri kufunga ukurasa wa kauli zake za uasharati na hivyo kuomba tu radhi kwa yale yaliyotokea? Mgombea huyo aliamua kulipiza kisasi, na kutoa wito katika mjadala wa mwisho kwa makahaba wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton katika mwaka mwaka 1990.

Matokeo ya kauli ya Bw Trump yameanza kujitokea. Wanawake leo wanamshtumu mgombea urais wa chama cha Republican aliwapapasa kimapenzi pila idhni yao. Katika gazeti la New York Times, wanasema, kama Jessica Leeds, kuwa wamelazimika kuzungumza hadharani baada yakuangalia mjadala uliyofanyika hivi karibuni kati ya Donald Trump na Hillary Clinton.

Sehemu hii mpya tayari imegonga vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari nchini Marekani.

Jessica Leeds alisafiri katika ndege moja na Donald Trump huku wakikaa kwenye viti viwili vinavyokaribiana "Nilishtushwa ghafla na kujihisi vibaya kuona mikono yake ikinigusa shemu mbalimbali za mwili. Ilikuwa ni kama pweza, kama vile alikua na mikono sita. Mikono yake ilikua kila mahali. Na wakati aliingiza mkono wake chini ya sketi yangu nilijihisi vibaya sana, nikaamua kukimbia, " Jessica Leeds amesema.

Mwanamke wa pili anasema Donald Trump alimkumbatia kimapenzi mwaka 2005 bila idhini yake wakati alikua akifanya kazi kama afisa wa mapokezi katika kampuni yaTrump Tower, inayomilikiwa na Donald Trump.

Donald Trump amekanusha kesi hizi zamani na kusemani njama za kutaka kumuangusha kisiasa, ili ashindwe katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwezi Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.