Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Trump na Clinton washambuliana katika mjadala mkali

Mjadala wa pili kati ya mitatu inayotarajiwa kati ya Donald Trump na Hillary Clinton umefanyika usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu. Mjadala huu ulikua mkali huku kila mmoja akijaribu kumshambulia mwingine.

Wagombea wawili Hillary Clinton na Donald Trump, wakiwasili katika Chuo Kikuu cha  St Louis, Marekani.
Wagombea wawili Hillary Clinton na Donald Trump, wakiwasili katika Chuo Kikuu cha St Louis, Marekani. REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Wagombea hao wawili katika uchaguzi wa urais kutoka vyama vya Republican na Democratic hawakupeana mkono kama ilivyokua katika mjadala wa kwanza, jambo lililodhihirisha chuki ambayo inaendelea kat ya wagombea hao.

Donald Trump amefutilia mbali madai ya kuwanyanyasa wanawake kingono, huku akimshambulia kwa hasira mume wa Hillary Clinton, Bill Clinton aliyekuwa rais wa Marekani.

Donald Trump ahata hivyo ametetea matusi aliyotoa kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu za siri kwa kumshambulia Hillary Clinton na mumewe.

Katika kanda ya video ya mwaka 2005 iliyosambazwa katika vyombo vya habari Ijumaa juma lililopita ilimfichua Trump akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu zao za siri.

Masuala la mzozo wa Syria, Uchokozi wa Urusi, na hatua ya bwana Trump kukata kutangaza malipo yake ya kodi na mpango wa Donald Trump wa ukaguzi mkali kwa wahamiaji wanaowasili kutoka mataifa yanayohusishwa na ugaidi yameibuka katika mjdala huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.