Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC

Colombia: Santos awasihi raia wake kuzingatia amani

Rais Juan Manuel Santos ameahidi kuwa 'amani nchini Colombia' 'imekaribia' baada ya kupokea wapinzani wa makubaliano na FARC Jumatano hii, wakati ambapo maelfu ya raia waliandamana wakidai mwisho wa vita.

Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos, na kiongozi wa kundi la waasi la FARC Timochenko,wakati wa sherehe ya kutia sani kwenye mkataba wa amani,Septemba 26, 2016 mjini Cartagena.
Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos, na kiongozi wa kundi la waasi la FARC Timochenko,wakati wa sherehe ya kutia sani kwenye mkataba wa amani,Septemba 26, 2016 mjini Cartagena. Colombian Presidency
Matangazo ya kibiashara

"Amani nchini Colombia imekaribia na tutafikia kwa hilo," Bw Santos amesema akiwa Ikulu mjini Bogota, baada ya majadiliano marefu na mpinzani wake mkubwa, Alvaro Uribe, kiongozi wa kampeni ya 'hapana' katika kura ya maoni ya Jumapili wakati ambapo wapiga kura walikataa mkataba wa amani na kundi la waasi la FARC.

Katika taarifa tofauti, Bw Uribe, aliyetawala nchi hiyo tangu mwaka 2002 hadi 2010 na kisha kuendesha kampeni dhidi ya waasi, amehakikisha kwamba 'ni bora amani kwa wananchi wote wa Colombia kuliko mkataba dhaifu kwa nusu ya wananchi'.

Bw Santos, ambaye aliapa kumaliza vita vilivyoiathiri chi yake kwa zaidi ya nusu karne, awali alikutana na rais mwingine wa zamani, Andrés Pastrana (1998-2002), mwanzilishi wa mazungumzo ya Caguan, jaribio lililopita la amani na kundi la waasi wa FARC.

Baada ya mkutano huo, Pastrana alisema aliomba kutekeleza 'mara moj' maeneo ambapo waasi watakusanyika ili kuweka chini silaha zao chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Alisema jambo hilo litawapatia matumani waasi wa kundi la FARC kwamba 'tutaendelea na mchakato huu'.

Rais Juan Manuel Santos amewapokea wapinzani wake ili kujaribu kuokoa makubaliano yaliyofikiwa kwa karibu miaka minne nchini Cuba na kundi la waasi la FARC), makubaliano ambayo yanazungumzia hasa upokonyaji silaha kwa waasi na kundi hilo kuwa chama cha kisiasa.

Bw Uribe amesema kunahitajika makubaliano mapya yatakayo wahusisha wananchi wote wa Colombia chini ya misingi ya sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.