Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Jean Ping awatolea wito wafuasi wake "kuendelea na msimamo wao"

Mvutano unaendelea kushuhudiwa nchini Gabon kati ya serikali na upinzani. Alhamisi hii, Septemba 29, Jean Ping amewatolea wito wafuasi wake kuendelea na msimamo wao wa kupinga uchaguzi wa Rais Ali Bongo, licha ya Mahakama ya Katiba kupasisha uchaguzi wake.

L'opposant gabonais Jean Ping, en meeting à Libreville, le 29 août 2016.
L'opposant gabonais Jean Ping, en meeting à Libreville, le 29 août 2016. AFP/Marco Longari
Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo kambi yake imepata pigo kubwa kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Katiba na kuapishwa kwa Ali Bongo, Jean Ping amesema kuwa bado ataendelea kupinga uchaguzi wa ali Bongo. Nyumbani kwake, mbele ya kamera huku wafuasi wake wakikusanyika karibu na bwawa la kuogelea, Jean Ping alikua akitabasamu, na kucheza muziki na wafuasi wake. Lakini wakati alipoanza kuzungumza na waandishi wa habari, ameonyesha kuwa bado msimamo wake haujabadilika. Jean Ping amesema analaani mapinduzi ya kijeshi dhidi ya uchaguzi, mapinduzi ambayo kwa mujibu wa JeanPing, yamefanywa na utawala. Kiongozi huyo wa upinzani ameonyesha dhamira kushikilia majukumu yake kama rais aliyechaguliwa.

Jean Ping amesema kuwa kamwe hatotambua ushindi wa Rais Ali Bongo ambaye, amesema mwanasiasa huyo, mikono yake imejaa damu za raia wa Gabon. Ima kuhusu serikali ya umoja uliopendekezwa na utawala, Jean Ping amefutilia mbali hoja hiyo. "Mazungumzo gani? Na nani, na kwa madhumuni gani? Angalia mtu ambaye amesusiwa na raia na kushindwa katika uchaguzi, ambaye anaomba yule aliyeibwa kura kuja kujadiliana pamoja naye. Anaomba hivyo akiwashikilia watu bunduki kichwani, huku akiamuru jeshi kuziweka sawa helikopta za mashambulizi na ndege za kivita juu ya nyumba zetu. Kamwe hatutoshiriki mazungumzo yoyote chini ya kivuli cha dikteta, " amesema Jean Ping.

Maneno haya ni tofauti na yale yaliyotamkwa saa chache na Waziri mkuu mpya. Emmanuel Issoze-Ndonget almethibitisha kuwa baraza la mawaziri litakualimeundwa hadi Jumapili. Amesema kuwa wanaendelea kuwasiliana kwa minajili ya kuunda serikali ya umoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.