Pata taarifa kuu
MAREKANI-DONALD TRUMP-HILLARY CLINTON

Hillary Clinton na Donald Trump wachuana katika mdahalo wa urais

Wagombea wa urais nchini Marekani Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican, wamechuana katika mdahalo wa kwanza wa Televisheni kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba mwaka huu.

Mdahalo wa kwanza uliyorushwa kwenye runinga kati ya Hillary Clinton na Donald Trump mjini New York Septemba 26, 2016.
Mdahalo wa kwanza uliyorushwa kwenye runinga kati ya Hillary Clinton na Donald Trump mjini New York Septemba 26, 2016. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa dakika 90 wagombea hao wawili walitoana kijasho mbele ya Mamilioni ya raia wa Marekani na watu wengine duniani, waliokuwa wanatazama mdahalo huo mjini New York.

Miongoni mwa maswala nyeti waliyojadili ni pamoja na namna ya kuimarisha uchumi wa Marekani, usalama hususan kupambana na ugaidi na vita vya Iraq.

Bi.Clinton aliyeonekana mtulivu wakati wa mdahalo huo, alimshutumu mpinzani wake kwa kukwepa kulipa kodi licha ya kudai kuwa yeye ni tajiri na mfanyibiashara mkubwa na kusema kuwa inaonekana Trump anaficha kitu.

Akijibu tuhma hizo, Trump alisema ni kweli ni mfanyibiashara na tajiri na kuongeza kuwa anajiona mwerevu kwa kufanikiwa kukwepa kulipa kodi.

Pamoja na hilo, alitaka kuwekwa wazi rekodi za maelfu ya barua pepe za Bi.Clinton ambazo zinadaiwa kufutwa wakati akiwa Waziri wa Mambo ya nje.

Trump amesema akijithathmini, na uzoefu alionao kama mfanyibiashara, anatosha kabisa kuwa rais wa Marekani kwa kile alichokieleza kuwa Marekani inamataka kiongozi kama yeye.

Clinton naye kwa upande wake amemwelezea Bwana Trump kama mtu ambaye hana uwezo wa kuongoza Marekani kutokana na matamshi yake, ikiwa ni pamoja na kuwadhalalisha wanawake na kuwafafanisha kama nguruwe.

Idadi kubwa ya raia wa Marekani watakaopiga kura na waliokuwa wanatazama mjadala huu, wamesema Hillary Clinton ndiye aliyeshinda katika mdahalo wa leo.

Wagombea hao watapambana tena katika midahalo mingine miwili kabla ya siku ya upigaji kura tarehe 8 mwezi Novemba.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.