Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Macky Sall ampongeza Ali Bongo

Rais wa Senegal ametuma ujumbe wa pongezi kwa Ali Bongo Ondimba, kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Katiba kuthibitisha kuwa Rais wa Gabon amechaguliwa kwa mara nyingine kwenye wadhifa huo

Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Macky Sall ni rais wa kwanza kumpongeza Ali Bongo baada ya Mahakama ya Katiba kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais ya Agosti 27.

Rais wa Senegal amesema ametuma ujumbe huo kwa niaba ya wananchi wa Senegal na kwa jina lake mwenyewe akisema "kumtakia mafanikio katika uongozi wake".

Katika taarifa yake, Rais wa Chad, Idriss Déby Itno, Rais wa sasa Umoja wa Afrika, aliwataka viongozi wa kisiasa wa Gabon "kuheshimu uamuzi wa Mahakam ya Katiba ya Gabon .

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alisema amesikia uamuzi wa Mahakama ya Katiba, ambayo ilithibitisha kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa Ali Bongo Ondimba.

Ban Ki-moon ameitoa wito kwa wanasiasa wa Gabon kuanzisha "mazungumzo mapana" kwa ajili ya utulivu nchini humo.

Kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa Bw Bongo kunapingwa na mwanasiasa wa upinzani Jean Ping, ambaye alijitangaza mwenyewe kuwa ni "rais aliyechaguliwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.