Pata taarifa kuu
BRAZIL-LULA

Rais wa zamani wa Brazil Lula kuhukumiwa kwa rushwa

Nchini Brazil, Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anatazamiwa kuhukumiwa kwa kosa la rushwa katika sehemu ya faili ya kambuni ya Petrobras, ikiwa ni kashfa kubwa ya rushwa katika historia ya Brazi, ambayo ilisababisha kuachishwa kazi kwa Rais Dilma Rousseff. Mshauri wake, Lula sasa anashtakiwa na anatazamiwa kufikishwa mbele ya majaji.

Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, wakati wa hotuba ya Dilma Rousseff.
Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, wakati wa hotuba ya Dilma Rousseff. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Sergio Moro, jaji anayehusika na uchunguzi, anaamini kuwa ana ushahidi wa kutosha, unaoonyesha kuhusika kwa Lula, anayeshtumiwa wakujitajirisha kinyume cha sheria na rushwa iliyokithir. Rais wa zamani alinufaika "moja kwa moja" hongo aliyokua akipewa na kampuni ya ujenzi BTP OAS, kwa zaidi ya Euro milioni moja. Mke wa Lula pia anashtumiwa kupokea fedha chafu, kama pamoja na viongozi kadhaa wa zamani wa kampuni ya OAS.

Viongozi kadhaa waandamizi wa kiuchumi na kisiasa wamehukumiwa kwa kifungo cha muda mrefu gerezani kwa ajili ya kupokea rushwa, zilizotolewa na viongozi wakampuni kubwa ya mafuta ya Brazi. Karibu Euro bilioni 2 zilipitishwa mlango wa nyuma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wakili wa Lula, Sergio Morro jaji anayehusika na uchunguzi, amepoteza umaarufu wake kutokana na kupendelea upande fulani.Amestumu mateso na ukosefu wa ushahidi dhidi ya rais wa zamani ambaye amekuwa alishtakiwa kwa kosa la kudharau vyombo vya sheria mwishoni mwa mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.