Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: kalenda ya uchaguzi itaanza na uchaguzi wa urais

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, upinzani umerudi kwenye meza ya mazungumzo baada ya makubaliano yaliyofikiwa kuhusu uchaguzi, baada ya mkutano wajumbe watano kutoka serikali na washirika wake pamoja na wajumbe wanne kutoka kambi ya upinzani.

Uchaguzi wa rais, wa wabunge na wa mkoa utafanyika mbalimbali DRC.
Uchaguzi wa rais, wa wabunge na wa mkoa utafanyika mbalimbali DRC. AFP PHOTO/ ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Inajulikana tangu Jumatano hii, Septemba 14 kwamba kalenda ya uchaguzi itaanza na uchaguzi wa rais.

Uchaguzi utaoanza ni ule wa urais, ufuate uchaguzi wa wabunge na baadaye uchaguzi wa mikoa. hayo ndio maelewano yaliyoafikiwa kati ya wajumbe hao. Kwa hiyo Tume ya Uchaguzi imepewa kazi ya kuchunguza kama kitaalam na kifedha, itawezekana kuandaa uchaguzi wa serikali za mitaa wakati mmoja na na chaguzi zote tatu.

Ujumbe wa kambi ya upinzani ulikua unataka uchaguzi wa urais ndio uanze. Uchaguzi huo utafanyika na chaguzi zingine tatu ikiwa kifedha na kiufundi itawezekana.

Kwa hiyo upinzani unarudi Alhamisi Septemba 15kwenye meza ya mazungumzo. Serikali na washirika wake wamesema walikubaliana "kwa maslahi ya taifa." Lakini hakuna tarehe iliyopangwa kwa ajili ya mzunguko huu wa kwanza wa uchaguzi. "Kuna ulazima wa kusubiri hadi daftari la uchaguzi likamilike," amesema Waziri wa Sheria, ambaye ni mmoja wa wasimamizi katika mazungumzo hayo kutoka upande wa serikali na washirika wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.