Pata taarifa kuu
GABON-USALAMA

Gabon: upinzani watolea wito raia kusalia makwao

Ijumaa usiku juma lililopita, Waziri Mkuu wa Gabon Daniel Ona Ondo aliwatolea wito raia kwenda kazini kuanzia Jumatatu Septemba 5. jana Jumapili, Upinzani badala yake umewatolea wito raia kusalia makwao.

Moshi mweusi juu ya anga ya mji wa Libreville.
Moshi mweusi juu ya anga ya mji wa Libreville. AFP/Marco Longari
Matangazo ya kibiashara

Kama meneja wa kampeni za Jean Ping anakubali kwamba itakua ni njia ya shinikizo kuushawishi utawala kuhesabu upya kura za uchaguzi katika kila kituo cha kupigia kurakatika mkoa wa Haut-Ogooué, René Ndemezo Obiang, kwa upande wake, anasema utaratibu huo ni katika hali ya kuwalinda raia kufuatia kukosekana kwa usalama wakati huu.

Katika hali ya kutetea wito huo kwa raia kusalia makwao, meneja wa kampeni za Jean Ping amesema kuwa hali ya usalama bado ni tete nchini Gabon baada ya ghasia ziloizofuata muda mchache tu baada ya kutangzwa Jumatano juma lililopita kwa matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Ali Bongo Ondimba. " Kuna watu waliyotoweka, barabara zimefungwa madaraja yamevunjwa nchini kote, mawasiliano ya simu yamekatwa. Kutokana na yote haya, haiwezekani kwa wananchi wa Gabon kwenda kufanya biashara zao. Yote haya kwanza ni usalama wa wananchi unaopewa kipaumbele, na ndio maana tumewatolea wito wananchi wa Gabon kusalia makwao, " amesema René Ndemezo Obiang.

vurugu ina abated lakini Gabon wanaishi katika wasiwasi na ukosefu wa habari. Jumapili internet ilikuwa bado kimya na kadhaa ya ndani vyombo vya habari walikuwa kuharibiwa na walikuwa unusable.

Aidha, meneja wa kampeni za mgombea aliyeshindwa anathibitisha kwamba hii ni njia ya kuishinikiza serikali ya Gabon ili kuandaa zoezi jipya la uhesabuji wa kura katika vituo vyote vya mkoa wa Haut-Ogooué, kama alivyoomba Jean Ping na Umoja wa Ulaya, Ufaransa na USA. Kulingana na matokeo yaliyotolewa na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (Cenap), Ali Bongo alichaguliwa kwa 49.80% ya kura dhidi ya 48.23% ya kura alizopata Jean Ping.

Kwa jumla, vurugu zilizofuatia tangazo la matokeo ya uchaguzi wa uraisyalisababisha watu saba kupoteza maisha, ikiwa ni pamoja na raia watano katika mji wa Libreville, mmoja katika mji wa Port-Gentil, mji mkuu wa kiuchumi, na askari polisi katika mji wa Oyem, kaskazini mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.