Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Miji mbalimbali ya Gabon yakumbwa na vurugu

Masaa kadhaa baada ya kutangazwa Ali Bongo kama msindi wa uchaguzi wa urais uliyofanyika Jumamosi juma lililopita nchini Gabon, makao makuu ya mpinzani wake mkuu Jean Ping yalivamiwa na vikosi vya usalama, usiku wa Jumatano Agosti 31 hadi Alhamisi Septemba 1.

Askari polisi wa Gabon wapiga doria katika mitaa ya Libreville baada ya kutangazwa Ali Bongo kama mshindi wa uchaguzi wa urais Agosti 31, 2016.
Askari polisi wa Gabon wapiga doria katika mitaa ya Libreville baada ya kutangazwa Ali Bongo kama mshindi wa uchaguzi wa urais Agosti 31, 2016. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya usalama nchini Gabon vimejaribu kuvamia makao makuu ya ofisi ya chama kikuu cha upinzani alfajiri ya kuamkia Alhamisi September Mosi, ambapo watu kadhaa walijeruhiwa, saa chache baada ya Rais Ali Bongo Ondimba kutangazwa mshindi.

Shambulizi hili limesababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi wamejeruhiwa, "baadhi wakiwa katika hali mbaya sana", kwa mujibu wa Jean Ping ambaye hayupo katika eneo la tukio.

Wakati huo huo, wafuasi wa upinzani nchini Gabon wamechoma moto jengo la bunge la nchi hiyo baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi wa Rais Uliofanyika siku ya Jumamosi dhidi ya mpinzani wake mkuu Jean ping.

Shambulizi hili limeendeshwa na helikopta pamoja na kikosi cha ulinzi wa rais.

Wafuasi wengi wa upinzani wamekua wamejificha ndani ya jengo la mpinzani Jean Ping. Miongoni mwao walikuepo viongozi wakuu wa upinzani. Afisa wa aliyekua akihusika na kampeni ya Jean Ping aliiambia RFI kuwa shambulizi hilo lilianza usiku wa manane (saa za kimataifa) huku akibaini kwamba watu wengi wameuawa katika shambulizi hili.

Akihojiwa na RFI, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi (Cenap) ambaye yuko mafichoni, ameeleza kwamba washambuliaji, ambao ni askari wanatumia silaha nzito za kivita, aina ya M-16, na Famas.

Angalau watu 19 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa Jean Ping.

Kwa upande wake, Msemaji wa serikali ya Gabon amehakikisha kwamba shambulio dhidi ya makao makuu ya Jean Ping limelenga "wahalifu" ambao walichoma moto jengo la Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.