Pata taarifa kuu
BRAZIL-MICHEL TEMER

Brazil: Rais Michel Temer aapishwa

Nchini Brazil, Michel Temer, kaimu rais tangu mwezi Mei ametawazwa kuwa rais wa nchi hiyo Jumatano hii Agosti 31. Wakati huo huo Rais wa Brazil Dilma Rousseff ameondolewa rasmi madarakani na Baraza la Seneti.

Michel Temer ametawazwa kuwa rais wa Brazil, Agosti 31 mjini Brasilia.
Michel Temer ametawazwa kuwa rais wa Brazil, Agosti 31 mjini Brasilia. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Bi Rousseff amekua akishtumiwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umma baada ya utaratibu wenye utata, unaohitimisha miaka 13 ya serikali ya mrengo wa kushoto katika nchi kubwa ya Amerika ya Kusini.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff ameondolewa madarakani Jumatano hii na Baraza la Seneti kwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umma baada ya utaratibu wenye utata, unaohitimisha miaka 13 ya serikali ya mrengo wa kushoto katika nchi kubwa ya Amerika ya Kusini.

Maseneta wengi zaidi ya theluthi mbili wmeipiga kura ya kufukuzwa kwa rais kutoka chama tawala cha mrengo wa kushoto aliyechaguliwa mwaka 2010, na ambaye amerejelewa kwenye nafasi yake na makamu rais wa zamani, ambaye ni hasimu wake, Michel Temer. Michel Temer ni kutoka chama cha PMDB cha mrengo wa kati kulia).

Kwa jumla ya wabunge 81, 61 wamepiga kura kwa ajili ya kutimuliwa kwake na 20 pekee walipiga kura ya hapana.

Maseneta pia wamekua wakitazamiwa kupiga kura, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mahakama Kuu (STF) Richard Lewandowski, ili kuamua kama Bi Rousseff, anakabiliwa na hatia ya kutenda "uhalifu wa majukumu" pia kupigwa marufuku ya kufanya kazi ya serikali kwa kipindi cha miaka minane.

Kiongozi huyu wa zamani, ambaye amekua akifuata zoezi la Maseneta kutoka nyumbani kwake katika Ikulu ya Alvorada akiambatana na mshauri wake, rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva, atatoa tangazo kwa vyombo vya habari kabla ya kuondoka mjini wa Brasilia kuelekea nyumbani kwake katika mji wa Porto Alegre, kusini mwa Brazilia, ambapo wanaishi binti yake nawajukuu zake wawili.

Makamu wake wa zamani Rais Michel Temer, 75, ambaye amefurahia uamuzi wa Baraza la Seneti wa kumtimua mamlakani Dilma Rousseff, ataapishwa wakati wa hafla fupi, kabla ya kufanya ziara nchini China kuhudhuria mkutano wa G20, ambapo atajaribu kurejesha picha nchi ya kwanza kiuchumi ya Amerika ya Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.