Pata taarifa kuu
BRAZILI-SIASA-UCHUMI

Hatma ya Dilma Rousseff kujulikana

Rais wa Brazil aliyesimamishwa, Dilma Rousseff, Jumatatu hii anatarajiwa kukutana uso kwa uso na wanasiasa wanaomtuhumu kwa rushwa, katika jaribio lake la mwisho la kesi ya kuondolewa madarakani inayomkabili kwenye baraza seneti, kesi ambayo huenda ikashuhudia ikimaliza utawala wa miaka 13 ya chama tawala cha mrengo wa kushoto.

Rais aliyesimamishwa Dilma Rousseff katika katika Ikulu ya Aurore, Agosti 18, 2016, katika mji wa Brasilia.
Rais aliyesimamishwa Dilma Rousseff katika katika Ikulu ya Aurore, Agosti 18, 2016, katika mji wa Brasilia. ANDRESSA ANHOLETE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii leo kiongozi huyo atalihutubia baraza la seneti kabla ya kufanyika kwa kura ya mwisho kuamua mustakabali wake, huku kila kitu kikionyesha kuwa wabunge hao watapiga kura ya ndio kumuondoa.

Rousseff mwenye umri wa miaka 68 hivi sasa, anatuhumiwa kuchukua fedha za mkopo toka Serikalini ili kuziba mapungufu yaliyokuwemo kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha mwaka 2014.

Shinikizo la kuondoka madarakani kwa Rais Rousseff linachochewa na gadhabu kubwa ya wananchi kutokana na hali mbaya ya uchumi iliyowahi kuikumba nchi hiyo katika historia yake, huku siasa mbaya na rushwa iliyozunguka kampuni ya mafuta ya uma ya Petrobras, ikiwa kama sumu kwenye utawala wake.

Rais huyu wa kwanza mwanamke kuongoza Brazil, atahutubia Seneti nusu saa kabla ya kupigwa kwa kura yenyewe, huku ikiwa haijulikani kama atatumia lugha kali dhidi ya baraza hilo analodai wabunge wake wamepanga njama za kutaka kuipindua Serikali yake.

Wabunge 54 kati ya 81 wanapaswa kupiga kura ya ndio ili kuidhinisha kuondolewa madarakani kwa Rais Rousseff.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.