Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UCHUMI

Afrika Kusini: Waziri apinga amri ya polisi

Waziri wa Fedha Afrika nchini Arika Kusini, Pravin Gordhan, amesema Jumatano hii Agosti 24 kwamba hatotekeleza amri ya polisi ya kumtaka aripoti Ijumaa kwenye makao makuu ya polisi, baada ya kumshuku kufichua siri za nchi.

Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Pravin Gordhan.
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Pravin Gordhan. wikipedia
Matangazo ya kibiashara

"Sina wajibu wa kisheria wa mimi kutekeleza amri hii ya polisi. Sintokwenda kwenye makao makuu ya polisi," amesema Pravin Gordhan katika taarifa yake.

Bw Gordhan anashukiwa kuwa alisimamiwa upelelezi wa viongozi wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na Rais Jacob Zuma, kupitia kitengo cha wizara yake. Madai ambayo Waziri Fedha wa wa Afrika Kusini amefutilia mbali.

Katika barua aliotuma Jumatano hii kwa Hawks, kitengo maalum cha polisi, Pravin Gordhan ameeleza kwamba kitengo cha uchunguzi kama inavyodaiwa kiliundwa na mamlaka ya kodi (SARS) ambayo aliongoza kati ya miaka ya 1999 hadi mwaka 2009 kwa idhini ya serikali ya wakati huo.

Waziri Gordhan amesema, mamlaka hii iliundwa kwa minajili ya kukabiliana kwa bora zaidi ukwepaji kodi.

"Kutokana na kile mimi najua, kitengo hiki kilitekeleza majukumu yake kwa kuheshimu sheria," amesema waziri.

Mwezi Machi, Bw Gordhan alikuwa tayari alipata vitisho kutoka kwa Hawks kuhusu kesi hii.

Rand ya Afrika Kusini imeanguka 4% dhidi ya dola ya Marekani baada ya taarifa hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.