Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Nicolas Sarkozy atangaza kuwania kiti cha urais mwaka 2017

Nicolas Sarkozy ametangaza kwamba atawania kiti cha urais mwaka 2017 katika kitabu kitakachotolewa Jumatano Agosti 24. Aliyekuwa Rais wa Ufaransa amethibitisha hayo kwenye twitter Jumatatu hii, Agosti 22.

Nicolas Sarkozy wakati wa mkutano na wakulima katika mji wa Alsace, Julai 9, 2016.
Nicolas Sarkozy wakati wa mkutano na wakulima katika mji wa Alsace, Julai 9, 2016. REUTERS/Vincent Kessler
Matangazo ya kibiashara

"Nimeamua kugombea urais mwaka 2017. Ufaransa inahitaji kupewa kila kitu," ameandika Nicolas Sarkozy katika kitabu hicho chenye kurasa 250 kitakachotolewa Jumatano wiki hii. Kitabo hicho kinajulikana kwa jina la " yote kwa Ufaransa". Kitabu hiki "hatua ya kuanzia," amesema rais wa zamani wa kwenye Twitter.

Hivyo, kama wakati alivyotaka kuzindua kurudi kwake katika siasa, Nicolas Sarkozyamepitia kwenye kitabu alichoandika kwa kuwaambia Wafaransa.

Nicolas Sarkozy anakuwa mgombea wa kumi na tatu kutangaza kuwania katika katika kura za msingi kwa chama cha mrengo wa kulia kwa kujaribu kurudi katika uongozi wa nchi alioupoteza zaidi ya miaka minne iliyopita.

Tangazo hili imemaliza mashaka katika kambi ya Ncolas sarkozy, ambapo baadhi ya wafuasi wake wamekua hawana imani ya kugombea tena kwa rais huyo wa zamani wa Ufaransa katika kinyang'anyiro cha urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.