Pata taarifa kuu
UTURUKI-ERDOGAN

Operesheni ya kamata kamata yaendelea Uturuki

Serikali ya Uturuki imetoa amri mbili Jumatano hii zinazowafuta kazi maafisa wa polisi zaidi ya 2,000 na mamia ya askari na maafisa wa mamlaka ya taifa ya technolojia ya habari na mawasiliano (BTK) katika uhusiano na jaribio mapinduzi lililoshindwa Julai 15.

Rais wa Uturuki Erdogan, Julai 22, 2016 mbele ya Wabunge wa Uturuki.
Rais wa Uturuki Erdogan, Julai 22, 2016 mbele ya Wabunge wa Uturuki. AFP PHOTO / TURKEY'S PRESIDENTIAL PRESS SERVICE / KAYHAN OZER
Matangazo ya kibiashara

Amri hizi zilizochapishwa katika jarida la serikalii, zinaendana na hali ya hatari, pia zinaagiza kufungwa kwa mamlaka ya mawasiliano ya hali ya juu (TIB).

Maafisa waliofukuzwa kazi ikiwa ni pamoja na maafisa wa polisi 2,300, mamia wa askari na wafanyakazi 196 wa BTK, wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na imam Fethullah Gulen, mhubiri aliye uhamishoni nchini Marekani, ambaye serikali ya Uturuki inamtuhumu kupanga na kuandaa jaribio la mapinduzi.

Kwa mwezi mmoja wa operesheni hii ya kamata kamata, maelfu ya maafisa wa vikosi vya usalama wamefutwa kazi na imefunga Shule nyingi, mashirika mengi na makampuni mbalimbali.

Pamoja na maelfu ya wafanyakazi kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi, zaidi ya watu 35,000 wamekamatwa, ambapo nusu yao wamekamatwa na wanazuiliwa kwa muda katika jela mbalimbali.

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu gerezani, serikali imechukua Jumatano hii amri nyingine inayoleta mageuzi ya mfumo wa kifungo cha nje. Kwenye akaunti yake ya Twitter, Waziri wa Sheria, Bekir Bozdag, amesema kuwa wafungwa 38,000 watafaidika na mfumo huo.

Askari wamkamata Sjenti Erkan Cikat, anayetuhumiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa la Julai 15, 2015 Uturuki.
Askari wamkamata Sjenti Erkan Cikat, anayetuhumiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa la Julai 15, 2015 Uturuki. REUTERS/Kenan Gurbuz

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.