Pata taarifa kuu
CHINA-AJALI

China: zaidi ya watu 21 wapoteza maisha katika mlipuko

Nchini China, mlipuko katika kiwanda cha makaa ya mawe umlisababisha watu wasiopungua 21 kupoteza maisha Alhamisi Agosti 11. wengine watano walijeruhiwa, kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka shirika la habari la serikali la Xinhua.

Mtazamo wa mlipuko kwa juu.
Mtazamo wa mlipuko kwa juu. People's Daily China
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea mchana katika kiwanda hicho katika mji wa Dangyang katika mkoa wa Hubei (katikati mwa nchi).

Moshi mnene mweusi ulifumba kwenye paa za kiwanda hicho cha Dangyang. Wakati huo huo mlipuko mkubwa ulisababishwa na kupasuka kwa mlingoti wa mvuke.

Picha zilizorushwa kwenye tovuti ya gazeti la kila siku la People's Daily China zinakukumbusha picha za vifo vingine viliyosababishwa na kuteketea kwa moto kwa bandari ya Tianjin. Tukio hili lilitokea Agosti 12, 2015. Zaidi ya tani 3,000 za kemikali, ziliteketea kwa moto, na watu 165 walipoteza maisha.

Katika usiku wa maadhimisho ya miaka ya kwanza ya janga hili, ajali nyingine imejiongeza kwa ile iliyotokea mwezi Agosti mwaka jana nchini China, nchi ambayo inajulikana kwa kushindwa kuzingatia sheria.

Mwezi Mei, mlipuko uliteketeza kiwanda betri za lithiamu katika jimbo la Jiangsu. Mwezi Aprili, katika mji wa Shenzhen, mlipuko ulishuhudiwa katika kiwanda cha kuzalisha unga wa alumini na kusababishwa vifo vya watu wanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.