Pata taarifa kuu
BRAZIL-DILMA ROUSSEFF

Brazil: Kamati ya Seneti yaidhinisha kesi ya Dilma Rousseff

Nchini Brazil, kamati ya Seneti, Alhamisi, Agosti 4, imepitisha uamuzi kuwa Dilma Rousseff afuatiliwe katika kesi inayomkabili ya utumiaji mbaya wa fedha za umma. Moja ya Hatua, kwa ajili ya kuondolewa mamlakani kwa Dilma Rousseff.

Hatma ya Dilma Rousseff kujulikana mwishoni mwa mwezi Agosti au mapema mwezi Septemba.
Hatma ya Dilma Rousseff kujulikana mwishoni mwa mwezi Agosti au mapema mwezi Septemba. EVARISTO SA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Seneti imepiga kura kwa idadi kubwa kwa muendelezo wa mashtaka dhidi ya rais wa Brazil. Maseneta wamekua wakijadili ripoti kuhusu uchunguzi uliyotolewa mwanzoni mwa wiki hii, ambayo ilihitimisha kuwa Dilma Rousseff amepatiakana na hatia, akishutumiwa kutumia fedha za umma ili aweze kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.

Kura ya mwisho ya Baraza la itapigwa, hata hivyo, mwezi Agosti au mapema mwezi Septemba. Wakati huo huo, mpinzani wake, aliyekuwa Makamu wa Rais Michel Temer, ataendelea kuwa rais wa mpito. Michel Temer ataongoza sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki, Dilma Rousseff ameshaamua kutohudhuria sherehe hizo.

Baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili mwaka 2014, rais wa Brazil aliondolewa madarakani na baraza la Seneti Mei 12. Bado anakanusha kuwa hajakiuka Katiba na anasema kuwa amefanyiwa mapinduzi ya kitaasisi yaliyoandaliwa na vyama vya mrengo wa kulia pamoja na wapinzani wake wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.