Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA

Tunisia: Waziri mwenye umri wa miaka 40 ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Waziri wa Mambo Ndani Chahed Youssef, mwenye umri wa miaka 40, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu, na ameahidi kupambana dhidi ya ugaidi, ufisadi na ukosefu wa ajira, kipaumbele chake katika nchi yenye mgogoro.

Beji Caid Essebsi Rais (kulia) na Youssef Chahed (kushoto) Agosti 3, 2016 katika Ikulu ya Rais ya Carthage.
Beji Caid Essebsi Rais (kulia) na Youssef Chahed (kushoto) Agosti 3, 2016 katika Ikulu ya Rais ya Carthage. AFP / Fethi Belaid
Matangazo ya kibiashara

Kama Bw Chahed na baraza lake la Mawaziri wataidhinishwa na Bunge, atakuwaWaziri Mkuu mwenye umri mdogo katika historia ya kisasa ya Tunisia.

"Leo hii, tunauingia katika hatua mpya ambayo inahitaji juhudi, kujitolea, ujasiri, kutokuwa na ubinafsi na ufumbuzi kutoka mfumo wa zamani," amesema Bw Chahed kwa waandishi wa habari katika ikulu ya Carthage, baada tu ya kuteuliwa rasmi na Rais Beji Caid Essebsi.

Uteuzi wa Bw Chahed unakuja baada ya Bunge kufuta imani Jumamosi kwa Waziri Mkuu Habib Essid, miezi 18 tu baada ya uteuzi wake.

Rais Essebsi alikuwa amesema Juni 2 kuunda serikali ya umoja wa kitaifa bada ya kukosolewa dhidi ya afisi ya Essid, akishtumiwa uzembe wakati ambapoTunisia inapitia kipindi nyeti pamoja na uchumi unaoelekea njia panda na kuwepo kwa vitisho vya wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.