Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Beijing yaomba Marekani kusitisha "uchochezi" katika Bahari ya China Kusini (Waziri wa Ulinzi wa China, Wei Fenghe)
Siasa - Uchumi

Maandamano mapya yafanyika Brazil

media Waandamanaji wakibebelea bango lililoandikwa "tunataka rais wa mpito wa Brazil Michel Temer aachie ngazi", Julai 31, 2016 Rio de Janeiro. REUTERS/Mariana Bazo

Siku tano kabla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki, maelfu kadhaa ya watu waliandamana Jumapili Julai 31 katika miji kadhaa nchini Brazil wakidai Rais Dilma Rousseff aondoke mamlakani moja kwa moja.

Makundi mengine ya watu yaliingia mitaani yakidai kumuunga mkono rais huyo aliyewekwa kando na kumtuhumu rais wa mpito Michel Temer.

Mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini Brazil, wakati nchi hii inajiandaa kuwa mwenyeji wa tukio kubwa duniani, huku mgawanyiko ukijitokeza kati ya wanaounga mkono Dilma Rousseff na wale wanaompinga.

Kambi ya ya watu wanaompinga Dilma Rousseff waliingia mitaani ili kuonyesha kuwa bado wana nguvu. Wafausi hao wakivalia nguo zenye rangi ya kijani na manjano, rangi ya bendera ya taifa la Brazil, waliandamana katika miji mikubwa mbalimbali, kama vile Recife, Salvador, Belo Horizonte, Rio de Janeiro na Sao Paulo, ili kudai kuondolewa mamlakani kwa Dilma Rousseff.

Rais aliyetengwa kwenye wadhifa wake, pia aliungwa mkono katika maandamano ya jana Jumapili. Maandamano makubwa yalishuhudiwa Jumapili Julai 31 katika miji mikubwa mbalimbali wakiomba kurudi kwa Dilma Rousseff na kuondoka kwa Michel Temer, rais wa mpito.

Mgogoro wa kisiasa bado unaendelea

Brazili sasa imegawanyika katika makundi mawili, na hivyo kusababisha hali ya taharuki kuendelea kutanda katika nchi hii ya Amerika ya Kusini. hayo yanajiri wakati zikisalia siku tano tu kabla ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana