Pata taarifa kuu
UGIRIKI-IMF-UCHUMI

IMF yaitetea Ugiriki kupewa mkopo

Mawaziri wa fedha wa kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro wasubiriwa Jumanne hii katika mji wa Brussels kukubaliana juu ya kutolewa kwa mkopo mpya kwa Ugiriki na nchi hiyo kusamehewa madeni. Shirika la Fedha Duniani (IMF) inataka mkopo huo utolewe bila masharti yoyote.

Bendera ya Ugiriki  juu ya jengo la Bunge Athens Mei 22, 2016.
Bendera ya Ugiriki juu ya jengo la Bunge Athens Mei 22, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Fedha Duniani limeongeza shinikizo kwa nchi za Ulaya siku moja kabla ya mkutano huo kwa kutoa waraka unaodai kupunguza mzigo wa madeni ya Ugiriki bila masharti. Ugiriki inaongoza kwa mzigo mkubwa wa madeni katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro, karibu 180% ya pato la ndani nchini humo.

Ni "muhimu kwa kutoa katika masoko ishara imara na yenye kuaminika kuhusu dhamira ya wakopeshaji wa kitaasisi kufanya madeni endelevu, ambayo yanaweza kuchangia kupunguza gharama za fedha," IMF imesisitiza.

Shirika la Fedha Duniani pia linaamini kwamba hatua za kupunguza deni zinapaswa kuwa muhimu mpaka mwaka 2040 na kuongezwa hadi 2060 kutokana na uwezekano mdogo ambapo Ugiriki inaweza kuwa imeshuhudia ukuaji mkubwa na kupata bajeti ya ziada kwa kipindi hicho.

Waraka huo wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) umetolewa wakati ambapo tofauti zimeibuka kati ya taasisi hiyo ya kimataifa na baadhi ya nchi za Ulaya, ikiwa ni pamoja Ujerumani, mkopeshaji wa kwanza wa Athènes, kuhusu hatua za kupunguza deni ambapo Ugiriki inapaswa kunufaika.

IMF inaamini kwamba hatua hizi zinapaswa kuamuliwa mara moja wakati ambapo Ujerumani inataka Ugiriki ionyeshe nia yake ya kutekeleza hatua ya kubana uchumi kabla ya kujikubalisha kusonga mbele juu swala hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.