Pata taarifa kuu
MAREKANI-VIETNAM-USHIRIKIANO

Rais wa Marekani Barack Obama ziarani Vietnam

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili siku ya Jumapili Mei 22 katika mji wa mkuu wa Vietnam, Hanoi, kwa ziara ya siku tatu wakati ambapo anatarajia hasa kuimarisha uhusiano wa biashara na mkakati na Vietnam.

Rais wa Marekani Barack Obama awasili Vietanam kuzungumzi biashara huria na usalama.
Rais wa Marekani Barack Obama awasili Vietanam kuzungumzi biashara huria na usalama. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya tatu kwa rais wa Marekani tangu mwisho wa vita vya Vietnam mwaka 1975, baada ya ile ya Bill Clinton na George W. Bush.

Baada ya ziara ya Bill Clinton na George W. Bush, hii ni ziara ya tatu kwa rais wa Marekani tangu kumalizika kwa vita (1975) inaongeza nguvu miongo miwili ya kufufuka kwa haraka kwa uhusiano ambao wengi wangeweza kufikiria haraka kutokana na ukubwa wa majeraha yaliyosababishwa na uhasama kati ya nchi hizi mbili.

Rais wa Marekani amepanga kufanya ziara ya siku tatu nchini Vietnam kwa sababu mbalimbali : mikutano baina ya viongozi muhimu wa nchi hizi mbili, hotuba, kukutana na vijana wa vietnam katika mji wa Ho Chi-Minh (zamani ikitwa Saigon)

Katika mji wa Hanoi, matarajio yanayozunguka ziara hii ya kwanza ya Bw Obama, ambaye anaondoka madarakani mapema mwaka 2017 ni mengi mno.

"Bado kuna baadhi ambao wana mashaka (na Washington) ndani ya wasomi wa Vietnam, lakini ongezeko la uthibitisho wa Beijing katika Bahari ya Kusini mwa China imeleta mabadiliko mionngoni mwa watu na kupelekea kufufuka kwa kasi uhusiano na Marekani, " Murray Hiebert, mchambuzi katika Kituo cha Mkakati na Mafunzo ya Kimataifa, amesema.

Kuna mvutano kati ya China na Vietnam kuhusu visiwa vya Paracels na Spratlys, katikati mwa njia ya majini ya kimataifa.

Katika suala la kiuchumi, nchi hizi mbili zina matumaini ya kuona unafikiwa haraka mkataba wa biashara huria (TPP) utakaosainiwa kati ya nchi 12 za Ukanda huo lakini bao Marekani inatiliwa mashaka kuwa huenda isisaini mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.