Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA

Moïse Katumbi arejea nyumbani baada ya kusikilizwa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Moïse Katumbi amesikilizwa kwa zaidi ya saa sita, Jumatano hii, Mei 11, katika ofisi ya mwendesha mashitaka mjini Lubumbashi. Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga anatuhumiwa kuajiri. Karibu na jengo la mahakama, wafuasi wake walitawanywa na polisi.

Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016.
Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016. © REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Moïse Katumbi ameondoka huru kutoka mahakamani saa 11:30 jioni. Lakini mvutano haukukomea hapo. Umati wa wafuasi wake walikuja kumsindikiza hadi nyumbani kwake, huku wakipiga mayowe "Katumbi rais". Hata hivyo umati huo wa wafuasi wake ulitawanywa na vikosi vya usalama.

Karibu saa 5:20 mchana, Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga aliwasili Mahakamani, huku akibebelea bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo juu ya suti yake nyeupe.

Polisi yawatawanya wafuasi wa Katumbi

Wakati aliingia mahakamani, polisi ilitawanya umati wa wafuasi wake bila kujali kinachoendelea, huku ikitumia mabomu ya machozi. Kwa mujibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali, watu kadhaa wamekamatwa. Mashirika hayo pia yanalaani vurugu zilizosababishwa na polisi. Lakini afisa mmoja wa polisi amejibu jioni hii: "Hakuna vurugu" na "wote wale waliokamatwa wameachiwa."

Licha ya mazingira haya, wafuasi wengi wa Moïse Katumbi walisalia pembezuni mwa Mahakama kwa muda wa saa sita alizosikilizwa.

Kwa upande wa utetezi wamebaini kwamba faili hiyo ni tupu. "Mwendesha ameomba maelezo ya ziada kuhusu kikao cha Jumatatu wiki hii na kuonyesha baadhi ya vyeti kama ushahidi kwa tuhuma dhidi ya Moïse Katumbi, lakini vyeti hivi pia ni vyenye utata kwa kuweza kuchukuliwa kama ushahidi, " mmoja wa wanasheria amesema.

Mahakama ya Katiba yatoa msimamo wake

Hayo yakijiri Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema Joseph Kabila anaweza kubaki katika wadhifa wake baada ya 2016 endapo uchaguzi wa rais hautafanyika mwaka huu (Mahakama ya Katiba)

Mahakama ya Katiba imetoa msimamo huo ikijibu barua iliyowasilishwa na vyama viliyoseikalini, huku matarajio ya kufanyika kwa uchaguzi mwaka 2016 yakisogezwa kila kukicha. Katika uamuzi wake iliyoutoa Jumatano, Mei 11, Mahakama ya Katiba ilisema: "Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anaweza kubaki katika wadhifa wake baada ya 2016 endapo uchaguzi hautafanyika mwaka huu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.