Pata taarifa kuu
UFILIPINO-UCHAGUZI

Rodrigo Duterte aibuka msindi katika uchaguzi wa urais

Mgombea anayependwa Rodrigo Duterte ameibuka mshindi wa uchaguzi wa urais, kwa mujibu wa PPCRV, taaisi ya Kanisa Katoliki inayofuatilia uchaguzi, iliyoruhusiwa na serikali ya Ufilipino kwa kukusanya matokeo.

Mgombea Rodrigo Duterte, Davao, Jumatatu Mei 9, 2016.
Mgombea Rodrigo Duterte, Davao, Jumatatu Mei 9, 2016. REUTERS/Erik De Castro
Matangazo ya kibiashara

Jumanne hii asubuhi, baada ya kuhesabu karibu 90% ya kura, Rodrigo Dulerte alikua ameshapata kura milioni 5.84mbele ya msindani wake wa karibu.

Jumatatu wiki hii Wafilipino walipiga kura kwa wingi mazungumzo tayari mashauriano yameanza kuhusu serikali ijayo. Rodrigo Duterte, mkuu wa jiji la Davao kusini mwa Ufilipino, alikuwa wa kwanza kujieleza Jumatatu hii jioni kuhusu ushindi huo. Katika hotuba yake, aliwambia wagombea wengine ameshinda katika uchaguzi wa urais, na kuwatolea wito "kuwa marafiki".

Baadaye, mtu wa pili alietoa msimamo wake kuhusu uchaguzi huo, ni Seneta Grace Poe ambaye alikubali kushindwa na kumpigia simu Rodrigo Duterte na kwa kumpongeza.

Pia, wito wa kuheshimu mchakato wa kidemokrasia umetolewa na mgombea Jejomar Binay, aliyekuwa makamu wa rais. Tangu kuanza kwa kampeni, wengi walihofia kutokea kwa machafuko iwapo matokeo yatapingwa.

Katika siku za hivi karibuni, Rodrigo Duterte alilengwa na mashambulizi. Washindani wake walimtuhumu kuwa mtu hatari kwa demokrasia.

Kwa upande wake, Rodrigo Duterte kupingwa na baadhi ya wajumbe katika chama tawala.Waziri wa Mambo ya Ndani, Mar Roxas, ameyataja matokeo haya kuwa "yanakatisha tamaa."

Katika hotuba yake, Rodrigo Duterte ameahidi kuyaangamiza makundi ya wahalifu ambayo yamekua sugu nchini Ufilipino, hasa katik mji wa Davao.

"Mumesahau sheria juu ya haki za binadamu," usisiti kumtaja yule aliyeua watu zaidi ya 1,000, " amesema Duterte.

"Kama nikichaguliwa kuwa rais, nitafanya hasa kile nilichofanya nilipokua mkuu wa jiji la Davao. Nyinyi, wafanyabiashara, majambazi, na wahalifu, ni bora kuondoka kwa sababu nitawaua, " ameongeza Rodrigo Dulerte.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.