Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA-UCHUMI

Mkanganyiko kuhusu hatima ya Rousseff

Spika wa Bunge la Brazil amefuta Jumatatu hii kwa mshangao mkubwa kura ya wabunge iliyopitisha Aprili 17 utaratibu wa kumng'atua mamlakani Rais Dilma Rousseff. Lakini jioni, hali ya mambo iligeuka. Rais wa Baraza la Seneti Renan Calheiros ameamuru kuendelea kwa utaratibu huo.

Dilma Rousseff, mwenyewe, amekiri kwamba hali kuhusu utaratibu wa kutimuliwa kwake mamlakani imekumbwa na hali ya sintofaham. Brasilia, Mei 9 2016.
Dilma Rousseff, mwenyewe, amekiri kwamba hali kuhusu utaratibu wa kutimuliwa kwake mamlakani imekumbwa na hali ya sintofaham. Brasilia, Mei 9 2016. REUTERS/Adriano Machado
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa Waldir Maranhao umeibua mkanganyiko amnapo Maseneta walitarajiwa kupiga kura wiki hii ufunguzi rasmi wa kesi ya kujiuzulu kwa Dilma Rousseff kutumia vibaya akaunti za sawa na kumuwekwa rais kando ya kwa kipindi cha miezi sita kwa kusubiri hukumu ya mwisho.

Waldir Maranhao amesema katika taarifa yake kwamba Baraza la Bunge litaanza upya utaratibu wa kumng'oa mamlakani ambao kwa sasa uko mikononi mwa Baraza la Seneti kwa kuweza kuendelea na kura mpya juu ya suala hilo.

Dilma Rousseff amesema kuwa rufaa ilikubalika dhidi ya zoezi la kura ya wabunge shughuli na kwamba mchakato wa wa kujiuzulu umesimamishwa. Ameongeza kuwa matokeo ya uamuzi huu kwa sasa hayakuwekwa wazi.

Wiki iliyopita, Maranhao alirejelea nafasi ya Eduardo Cunha katika uongozi wa Baraza la Bunge. Eduardo Cunha alisimamishwa kwenye nafasi hiyo na Mahakama Kuu ya nchi katika uchunguzi kuhusu wa kesi za rushwa. Mpinzani mkuu wa Dilma Rousseff, Eduardo Cunha ni mmoja wa Wabunge walioanzisha utaratibu wa kumng'atua rais wa Brazil.

Bunge la Brazil lilipiga kura Aprili 17 katika neema ya kumng'oa mamlakani Rais Dilma Rousseff anayeshtumiwa kutumia akaunti za umma kwa kuendeleza kuchaguliwa kwake upya mwaka 2014. Baada ya kuhesabu kura, wabunge 367 walipiga kura katika neema ya kumng'oa madarakani Rais Dilma Rousseff, uamuzi ambao ungelipitishwa na theluthi mbili ya kura sawa na kura 342 za Wabunge.

Rais wa Baraza la Seneti aamuru kuendelea kwa utaratibu wa kumng'oa rais

Mvutano umeendelea kujitokea kuhusu utaraibu wa kumng'atua mamlakani raisa wa Brazili Dilma Rousseff. Baada ya Kaimu Spika wa Bunge kuchukua hatua ya kufuta kura ya wabunge kuhusu utaratibu wa kumtimua rais Dilma Rousseff, hatimaye Rais wa Baraza la Seneti Renan Calheiros ameamuru kuendelea kwa mchakato wa kumtumua rais madarakani. Licha ya kelele za Maseneta wa mrengo wa kushoto, Rais wa Baraza la ameonekana ni mwenye msimamo thabiti. Ameamuru kuendelea kwa mchakato wa kumng'atua mamlaka Rais Dilma Rousseff, akisema "kutokua na muhimu wowote" uamuzi wa Kaimu Spika Bunge.

Hali ya wasiwasi imeendelea kuibuka nchini Brazil. Baraza la Seneti linajiandaa kupiga kura Jumatano wiki hii, Rais wa baraza hilo ameahidi. Kama Maseneta watapiga kura katika neema ya ya kumuangusha rais, Dilma Rousseff atasimamishwa mamlakani kwa miezi sita kwa kusubiri hukumu ya mwisho. Lakini Mahakama Kuu bado itajadili uamuzi wa Kaimu Spika wa Bunge wa kufut kura ya wabunge. Jambao lolote laweza kutokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.