Pata taarifa kuu
UFILIPINO-UCHAGUZI

Uchaguzi mkuu wafanyika Ufilipino

Wapiga kura nchini Ufilipino wanachagua rais mpya Jumatau hii na viongozi wengine huku mgombea ambaye ni meya Rodrigo "Digong" Duterte akitarajiwa kupata ushindi.

Wafuasi wa Rodrigo Duterte wakipokea fulana zenye picha ya mgombea siku moja kabla ya uchaguzi. Davao Mei 8 2016.
Wafuasi wa Rodrigo Duterte wakipokea fulana zenye picha ya mgombea siku moja kabla ya uchaguzi. Davao Mei 8 2016. REUTERS/Erik De Castro
Matangazo ya kibiashara

Wagombea watano wamejitokeza lakini Bwana Duterte anapewa nafasi kubwa ya kushinda licha ya matamshi makali kipindi cha kampeni na msimamo wake mkali.

Kampeni zilitawaliwa na masuala ya uchumi usawa na tatizo la rushwa.

Usalama umeimarishwa ili kukabiliana na uvunjifu wa amani wa aina yoyote katika zoezi hilo.

Zaidi ya maafisa usalama laki moja wamesambazwa ili kushika doria nchini humo wakati huu ripoti zikitaja watu 15 kuuawa katika kipindi cha kampeni.

Rais Benigno "Noynoy" Aquino anamaliza muda wake wa kukaa madarakani kwa mujibu wa katiba inayomtaka kuhudumu kwa muhula mmoja wenye miaka sita.

Wafilipino watapiga kura pia kuwachagua makamo wa rais na viongozi wa serikali za mitaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.