Pata taarifa kuu
IRAQ-SIASA

Hali ya taharuki yatanda Iraq

Iraq imetumbukia katika mgogoro mkubwa Jumanne hii wakati ambapo kikao cha Bunge kilikumbwa na hali ya sintofahamu, huku kukishuhudiwa maandamano makubwa katika mji wa Baghdad.

Wanamgambo wa vuguvugu la Sadr, jina la kiongozi wa Kishia Moqtada Sadr wakiandamana Baghdad Aprili 26, 2016.
Wanamgambo wa vuguvugu la Sadr, jina la kiongozi wa Kishia Moqtada Sadr wakiandamana Baghdad Aprili 26, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wamekua wakidai kuundwa haraka kwa serikali mpya ili kutekeleza mageuzi ya kupambana na rushwa.

Katika kikao cha Bunge cha Jumanne hii mjini Baghdad ambapo Wabunge walitarajia kupia kura ya imani kwa timu mpya ya mawaziri, baadhi ya Wabungewalimzuia Waziri Mkuu Haidar al-Abadi, kujieleza , huku wakimrushia machupa ya maji , kwa mujibu wa mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Pia Wabunge hao wamemkashifu Spika wa Bunge Salim al-Juburi, na kumtaja kushikilia wadhifa huo "kinyume cha sheria: huku wakipiga kelele "Salim, nje, nje!".

Kikao hicho kilihamishwa sehemu nyingine, mbunge huyo ameongeza, lakini Wabunge waliokua wakipinga kikao hicho, walikataliwa kuingia, hii ikiwa na maana kuwa uamuzi wowote utakaochukuliwa utapingwa.

Bw Abadi amekua akijaribu kwa muda wa wiki kadhaa kuunda serikali mpya ili kuchukua nafasi ya mawaziri kutoka baadhi ya vyama, na zaidi, kutekeleza mageuzi ya kupambana na rushwa, mageuzi ambayo yalipitishwa mwaka 2015, baada ya maandamano makubwa ya raia dhidi ya uzembe.

Lakini mapendekezo ya mabadiliko yalikataliwa na vyama vinavyoshikilia wizara mbalimbali ili kuhakikisha ulinzi wao na fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.