Pata taarifa kuu
CHAD-IDRISS DEBY

Idriss Déby achaguliwa tena, kwa mujibu wa matokeo ya awali

Nchini Chad, matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais wa Aprili 10 yametangazwa. Rais anayemaliza muda wake Idriss Deby amechaguliwa tena katika duru ya kwanza kwa 61.56% ya kura zote zilizopigwa. Ushiriki ulifikia katika kiwango cha 76.11%.

Rais wa Chad Idriss Déby achaguliwa kwa mara nyingine tena.
Rais wa Chad Idriss Déby achaguliwa kwa mara nyingine tena. AFP PHOTO / MIGUEL MEDINA
Matangazo ya kibiashara

Laoukein Kourayo Médard bila shaka ni ufunuo wa uchaguzi huu. Meya wa Moundou alienda mbali, zaidi ya mji wa pili wa nchi hiyo, na kufanikiwa hasa kusini mwa Chad, kwa kushikilia nafasi ya tatu kwa 10.69% ya kura.

Kiongozi wa upinzani Saleh Kebzabo ametoka wa pili kwa kura 12.80 % baada ya kupata kura nyingi katika mikoa miwili ya kusini magharibi, ambayo ni ngome zake.

Ingawa amchaguliwa tena katika duru ya kwanza, Idriss Deby ameanguka katika suala asilimia. Mwaka 2011, Idriss Deby alichaguliwa kwa zaidi ya 88% ya kura. Katika uchaguzi wa mwaka huu ameibuka msindi kwa 61.56%.

Waziri Mkuu wa zamani Djimrangar Dadnadji, ambaye alijiondoa katika chama tawala zaidi ya mwaka mmoja uliopita, amepata zaidi ya 5% ya kura. Wagombea wengine katika uchaguzi huo ambao ni pamoja na Malloum Yoboide, Brice Guedmbaye Mbaimon na Clement Djimet Bagaou - wote walio na umri ulio chini ya miaka 45 - kuishia kupata zaidi ya 1%. Wagombea wanaosalia, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani Coumakoye Kassiré, wamepata chini ya 1%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.