Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Ted Cruz amuangusha Trump Wisconsin

Wakati ambapo kura za mchujo zikiendelea katika majimbo mbalimbali ya Marekani, mgombea urais kutoka chama cha Republican Ted Cruz ameibuka mshindi na kumuangusha mshindane wake Donald Trump katika jimbo la Wisconsin.

Seneta wa Texas Ted Cruz, baada ya ushindi wake katika jimbo la Wisconsin, Jumanne, Aprili 5, 2016 katika mji wa Milwaukee.
Seneta wa Texas Ted Cruz, baada ya ushindi wake katika jimbo la Wisconsin, Jumanne, Aprili 5, 2016 katika mji wa Milwaukee. REUTERS/Kamil Krzaczynski
Matangazo ya kibiashara

“Leo ni siku muhimu sana, inatoa ujumbe kwa watu wa Marekani,” Bw Cruz amewaambia wafuasi wa chama hicho Milwaukee.

Licha ya pigo alilolipata katika kura hizi, Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na katika kura za maoni chama cha Republican.

Hata hivyo kuna wasiwasi kwamba huenda akashindwa kupata wajumbe wa kumuwezesha kuidhinishwa moja kwa moja kuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha Republican.

Bw Trump amekua akikosolewa kwa maneneo makali aliokua akitoa wakati wa kampeni zake za kusaka tiketi ya kupandisha bendera ya chama cha Republicana katika uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Hayo ya kijiri, Bernie Sanders mgombea urais wa chama cha Democratic amepata ushindi mkubwa dhidi ya Hillary Clinton. Hillary Clinton kwa sasa anaongoza kwa wajumbe.

Ushindi wa Sanders katika jimbo la Wisconsin umemuongezea nguvu kabla ya mchujo muhimu unaotazamiwa kufanyika katika majimbo ya New York na Pennsylvania.

Sanders ameewahkikishi wafuasi wake kwamba atabadilisha mambo kutokana na jinsi kampeni yake inavyoendelea.

"Mabadiliko kamili hayafanyiki kutoka juu kwenda chini, bali yanatoka chini kwenda juu,” Sanders amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.