Pata taarifa kuu
UKWEPAJI KODI-AFRIKA-ULAYA-ASIA-AMERIKA

"Panama Papers": ufunuo kuhusu kashfa ya kimataifa ya ukwepaji kodi

Tangu Jumapili usiku, vyombo vya habari duniani kote vimeanza kuchapisha taarifa kuhusu mali zilizofichwa na viongozi mbalimbali kutoka duniani kote. Marais wengi ambao wanashikilia madaraka kwa sasa wametajwa katika nyaraka za siri ambazo zimetumwa kwa waandishi wa habari 370 na vyumba vya habari 107.

Rais pekee kutoka mataifa ya Afrika anayehusishwa moja kwa moja katika kashfa ya ukwepaji kodi ni rais wa zamani wa Sudan Ahmed al-Mirghani, ambaye alifariki mwaka 2008.
Rais pekee kutoka mataifa ya Afrika anayehusishwa moja kwa moja katika kashfa ya ukwepaji kodi ni rais wa zamani wa Sudan Ahmed al-Mirghani, ambaye alifariki mwaka 2008. © AFP PHOTO/ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Inasemekana kuwa huo ni uvujaji mkubwa wa siri katika historia ya uandishi wa habari. Kesi hii ni kubwa mara kumi kuliko ile ya Offshore Leaks iliyogunduliwa mwaka 2013, inawakilisha jumla ya nyaraka milioni 11.5. Baadhi ya data zinatoka nyaraka za kale za ofisi maalum nchini Panama inayohusika na kuchunguza makampuni ya Offshore ya Mossack Fonseca.

Nyaraka hizi nyingi, ambazo zina barua pepe, maelezo, maubao, fax, zimetolewa na chanzo ambacho hakikutajwa jina katika gazeti la kila siku la Ujerumani la Süddeutsche Zeitung. gazeti hili limeshirikiana na vyumba vya habari vingine 106 duniani kote na kwa makubaliano Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari wanaojihusisha na utafiti mjini Washington. Tangu Jumapili, Aprili 3, magazeti hayo yanachapisha taarifa ambazo zinaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya viongozi.

Wakuu wa nchi kumi na mbili, ikiwa ni pamoja na sita ambao bado wanashikilia madaraka wamewekwa hatarini. Pia kuna mabilionea, vigogo katika michezo kama vile mchezaji wa soka Lionel Messi au Michel Platini. Wote wanaaminika kuwa walitumia ujanja wa offshore kwa kuficha mali zao. Miongoni mwa majina yaliyotajwa ni pamoja na Nawaz Sharif, Waziri Mkuu wa Pakistan, mfalme wa Saudi Arabia Salman, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, mwenzake wa Argentina Mauricio Macri, au Waziri Mkuu wa Icelandic, nk.

Watu wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin pia wanakabiliwa na kashfa hii. Nyaraka hii zinaonyesha jinsi marafiki wa rais wa Urusi walijilimbikizia mapesa mengi kutoka fedha za umma na kuzipeleka nje ya nchi.

Viongozi wa Afrika wahusishwa

Rais pekee wa zamani wa Sudan al-Mirghani, ambaye alifariki mwaka 2008, anahusishwa moja kwa moja katika kashfa hiyo. Hata hivyo, kuna watu wa karibu wa viongozi sita, kama mpwa wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, mjane wa Rais wa zamani wa Guinea Lansana Conté na katibu binafsi wa mfalme wa Morocco.

Mawaziri kadhaa na viongozi waandamizi pia wametajwa, ikiwa ni pamoja Jaynet Kabila Kyungu, Mbunge na dada wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Waziri wa wa Viwanda na Madini wa Algeria, Emmanuel Ndahiro, mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi nchini Rwanda au Bruno Jean-Richard Itoua Waziri wa utafiti wa Congo-Brazzaville. Pia kuna kesi inayomkabili wakati huu Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.