Pata taarifa kuu
IRAQ-SERIKALI MPYA

Iraq: Abadi apendekeza serikali mpya

Kiongozi wa Kishia mwenye ushawishi mkubwa nchini, Muqtada al-Sadr, ametoa wito kwa wafuasi wake Alhamisi hii, Machi 31 kumaliza mgomo unaodumu wiki mbili sasa mbele ya maeneo ya mapumziko mjini Baghdad, wakidai marekebisho katika serikali.

Wafuasi wa Imam Moqtada al-Sadr wakiadhimisha mwisho wa mgomo wao pamoja na vikosi vya usalama vya a Iraq Machi 31 2016.
Wafuasi wa Imam Moqtada al-Sadr wakiadhimisha mwisho wa mgomo wao pamoja na vikosi vya usalama vya a Iraq Machi 31 2016. REUTERS/Ahmed Saad
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limekuja baada ya Waziri Mkuu Haidar al-Abadi kuwasilisha Bungeni pendekezo la serikali mpya. Ilikuwa ni moja ya hatua zilioombwa na kiongozi wa Kishia.

Moqtada al-Sadr ametumia ushawishi wake wote ili kufanikisha ombi lake. Alishiriki mwenyewe katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa mbele ya maeneo ya mapumziko "maeneo ya kijani", ukiwa na kauli mbiu: mwisho wa ufisadi na uundaji wa serikali ya watu wenye uzoefu. Alikua ametishia kwenda kupambana na serikali iliopo.

Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Ulinzi waendelea kushikilia nafasi zao

Alhamisi mchana, Haidar al-Abadi, waziri Mkuu chini ya shinikizo la waandamanaji, alijaribu kukidhi mahitaji haya kwa kutangaza serikali mpya. Serikali yenye idadi ndogo ya mawaziri, kwa lengo la kuvunja mfumo wa kugawana madaraka uliopo tangu mwaka 2003 mfumo unaotuhumiwa kuweka mbele rushwa na uzembe.

Serikali hii itaundwa na watu huru wenye uzoefu katika nyanja mbalimbali. "Watu hawa tayari wameteuliwa, na wamechaguliwa kulingana na ujuzi na uadilifu wao", Waziri Mkuu wa Iraq amesema. Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dohuk, kutoka ukoo wa mfalme wa Iraq aliefariki mwaka 1958 ni mongoni mwa mawaziri waliopendekrzwa na Waziri Mkuu ... Majina kumi na sita yaliopendekezwa si watu kutoka moja kwa moja katika vyama vya kisiasa. Mawaziri wawili tu wameendelea kushikilia nafasi zao, ule wa Mambo ya Ndani na ule wa Ulinzi. A-Abadi amebaini kwamba kuteua mawaziri wapya kwenye nafasi hizo kunaweza kudhoofisha kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.