Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-KASHFA-ZUMA-UCHUNI

Afrika Kusini: upinzani waanzisha utaratibu wa kumng'oa Zuma mamlakani

Mahakama ya Katiba imeamua Alhamisi hii, Machi 31 kwamba Rais wa Afrika Kusini alikiuka katiba kwa kukataa kulipa fedha za umma zilizotumiwa kwa kukarabati makazi yake binafsi ya Nkandla.

Wajumbe wa upinzani wa kisiasa wakisikiliza kwa makini hukumu ya Mahakama ya Katiba dhidi ya Rais Zuma katika mji wa Johannesburg, Machi 31, 2016.
Wajumbe wa upinzani wa kisiasa wakisikiliza kwa makini hukumu ya Mahakama ya Katiba dhidi ya Rais Zuma katika mji wa Johannesburg, Machi 31, 2016. © REUTERS/Felix Dlangamandla/Pool
Matangazo ya kibiashara

Hii ni kashfa kubwa katika muhula wake: matumizi ya zaidi ya Euro milioni kumi na tano ya fedha za umma kwa maslahi yake binafsi. Kashfa zilio wazi zimeanza kuonekana katika kambi ya rais.

Shinikizo limeendelea kuongezeka kwa Rais Jacob Zuma, baada ya uamuzi wa Mahakam ya Katiba. Baada ya miaka kadhaa upinzani ukipambana mahakamani kuhusu kesi hii, hatimaye umefanikiwa. Rais atapaswa kurejesha fedha zilizotumiwa kwa kukarabati makazi yake binafsi. Lakini hasa, mahakama ya juu nchini humo imebaini kwamba Rais Jacob Zuma alikiuka katiba.

Julius Malema, kiongozi wa chama chenye msimamo mkali, ambaye amewasilisha mashitaka, amesema chama tawala kinapaswa kumchukulia hatua kali Rais Zuma. "Kama hawatafanya hivyo, tutakwenda Bungeni na kuomba ang'atuliwe mamlakani. Na kwa wakati huu, tunakata Rais Zuma kuja kujieleza mbele ya Bunge. Tutamsimamisha moja kwa moja, na tumsukume, ndiyo, tutamsukuma kwa sababu, kwa sasa si tena Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini". Malema ametoa wito kwa raia wa Afrika Kusini kuingia mitaani.

Chama kingine cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimetangaza kwamba kimeanzisha utaratibu wa kumng'atua Zuma mamlakani. "Mahakama ya Katiba imekuwa wazi: rais ameshindwa katika wajibu wake wa kulinda Katiba ya nchi hii, Mmusi Maimane, kiongozi wa chama cha DA amebaini. Katika masharti haya, ni jinsi gani Bunge linaweza kuendelea kutetea mtu ambaye hakuweza kuheshimu kiapo chake na kutetea Katiba yetu? Bunge haliwezi kufanya hivyo. Na tunataka Bunge kuchukua hatua mwafaka. "

Kwa mujibu wa Mmusi Maimane, wabunge kutoka chama cha ANC kuchukua jukumu lao.

Chama cha ANC chagawanyika

Chama cha ANC, kwa upande wake, kimebaini kwamba kitaheshimu uamuzi wa mahakama ya Katiba na kutathmini uamuzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.