Michezo mbalimbali kufanyika katika tamasha la watanzania wanaotumia mtandao wa Twitter
Watanzania watumiaji wa mtandao wa Twitter wanakutana kesho katika tamasha litakalohusisha mambo mbalimbali ikiwemo michezo.
Imechapishwa:
Tamasha hilo litafanyika katika Viwanja vya posta vilivyopo Kijitonyama Mjini Dar es Salaam.
Hili litakuwa tamasha la tatu tangu kuasisiwa kwake mwaka mmoja uliopita likiratibiwa na mmoja wa waasisi wake Fred Kavishe.
Mbali na michezo kama riadha, soka pia kutakuwa na huduma mbalimbali ikiwemo za elimu ya haki za binadamu itakayotolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania, LHRC na taasisi nyingine zikiwemo za kibenki.
Tayari kumekuwa na tambo mbalimbali kupitia mtandao wa Twitter ambapo watumiaji wamekuwa wakielezea hisia zao kuelekea tamasha hilo.
Waziri wa Viwanda wa Tanzania Innocent Bashungwa ametumia ukurasa wake wa Twitter kuonyesha nia ya kuhudhuria tamasha hilo