Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Soka: Lionel Messi atunukiwa taji ya mchezaji bora na kuweka rekodi mpya

media Lionel Messi mchezaji nyota wa Argentina, mshambuliaji wa FC Barcelona, ameshinda kwa mara ya sita 6 tuzo ya mchezaji bora duniani (Ballon d'Or) Jumatatu, Desemba 2, 2019. Susana Vera/Reuters

Nyota katika mchezo wa Soka nchini Argentina, Lionel Messi ameibuka mshindi wa taji ya Ballon d'Or 2019 na kuchukuwa kinyan'anyiro cha mchezaji bora duniani kwa mara ya sita, na hivyo kuweka rekodi mpya.

"Kiwango" kilichowekwa mwaka 2008 kimefikiwa. Mwaka jana Luka Modric alishinda kinyang'anyiro cha mchezaji bora duniani na kutunukiwa taji ya Ballon d'Or alipokuwa akiichezea Real Madrid, mshindi wa Ligi ya Mabingwa. Kiungo huyo wa kati alisitisha miaka kumi ya kutawaliwa kwa taji hiyo kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo (ambao kila mmoja ameshinda taji ya Ballons d'Or mara tano kati ya mwaka 2008 na 2017, (tazama orodha hapo chini).

Lionel Messi, 32, amenyakua tuzo hiyo baada ya kuikosa toka mwaka 2015 na hii ni kutokana na kuweza kufunga mara 54 katika klabu ya nchini kwake kwa mwaka 2018-2019 .

Tuzo ya Ballon d'Or imekuwa ikitolewa nchini Ufaransa kila mwaka toka 1956, na mshindi wake wa kwanza alikuwa mchezaji kutoka Uingereza Stanley Matthews.

Awali tuzo hiyo ilikuwa ni kwa wachezaji wa Ulaya tu kabla ya kufanyika mabadiliko mwaka 1995 na kujumuisha wachezaji wa mataifa yote duniani, mradi wanasakata kandanda katika vilabu vya Ulaya.

ORODHA YA WACHEZAJI WALIOTUNUKIWA TUZO YA BALLON D'OR KWA WANAUME 2019

1: Lionel Messi (Argentina / FC Barcelona)

2: Virgil van Dijk (Uholanzi / Liverpool)

3: Cristiano Ronaldo (Ureno / Juventus)

4: Sadio Mané (Senegal / Liverpool)

5: Mohamed Salah (Misri / Liverpool)

6: Kylian Mbappé (Ufaransa / PSG)

7: Alisson Becker (Brazil / Liverpool)

8: Robert Lewandowski (Poland / Bayern Munich)

9: Bernardo Silva (Ureno /Manchester City)

10: Riyad Mahrez (Algeria / Manchester City)

11: Frenkie de Jong (Uholanzi / Ajax Amsterdam

WASHINDI 15 WA TAJI YA BALLON D'OR KWA WANAUME

2019: Lionel Messi (Argentina / FC Barcelona)
2018: Modric ya Luka (Kroatia / Real Madrid)
2017: Cristiano Ronaldo (Ureno / Real Madrid)
2016: Cristiano Ronaldo (Ureno / Real Madrid)
2015: Lionel Messi (Argentina / FC Barcelona)
2014: Cristiano Ronaldo (Ureno / Real Madrid)
2013: Cristiano Ronaldo (Ureno / Real Madrid)
2012: Lionel Messi (Argentina / FC Barcelona)
2011: Lionel Messi (Argentina / FC Barcelona)
2010: Lionel Messi (Argentina / FC Barcelona)
2009: Lionel Messi (Argentina / FC Barcelona)
2008: Cristiano Ronaldo (Ureno / Manchester United)
2007: Kaka (Brazil / AC Milan)
2006: Fabio Cannavaro (Italia / Juventus & Real Madrid)
2005: Ronaldinho (Brazil / FC Barcelona)
2004: Andriy Shevchenko (Ukraine / AC Milan)
2003: Pavel Nedved (Jamhuri ya Czech / Juventus)
2002: Ronaldo (Brazil / Inter Milan & Real Madrid)
2001: Michael Owen (England / Liverpool)
2000: Luis Figo (Ureno / FC Barcelona & Real Madrid)

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana