Pata taarifa kuu
MIGNE-EQUATORIAL GUINEA-SOKA

Sebastien Migne ataeuliwa kuwa kocha mpya wa Equatorial Guinea

Mfaransa Sebastien Migne, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka wa Equatorial Guinea.

Kocha mpya wa Equitorial Guinea Sebastine Migne Novemba 07 2019
Kocha mpya wa Equitorial Guinea Sebastine Migne Novemba 07 2019 www.africatopsports.com
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya hapo, Migne alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Kenya lakini alifutwa kazi mwezi Agosti, baada matokeo mabaya wakati wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika AFCON, mwezi Julai nchini Misri lakini pia baada ya kuondolewa na Tanzania katika michuano ya kufuzu kucheza fainali ya CHAN mwaka 2021.

Migne atakumbukwa sana nchini Kenya kwa kuiwezesha Harambee Stars kufuzu katika michuano ya AFCON baada ya miaka 15.

Hata hivyo, amekabidhiwa mikoba ya Nzalang Nacional, ambayo inaorodheshwa katika ya 135 duniani katika ubora wa mchezo wa soka na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Mwaka 2015, wakati Equatorial Guinea ilipokuwa mwenyeji wa michuamo ya bara Afrika, ilimaliza katika nafasi ya nne na kupanda hadi katika nafasi ya 49 duniani wakati huo.

Kazi kubwa inayomsubiri rais kocha Migne ni kuisaidia timu hiyo kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon.

Mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Tanzania, jijini Dar es salaam tarehe Novemba tarehe 11.

Mbali na Tanzania, Equitorial Guinea imepangwa pamoja na Tunisia na Libya katika kundi J.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.