Pata taarifa kuu
KENYA-MICHEZO-MARAHON

Kosgei avunja rekodi katika mbio za Marathon akiwa na umri mdogo

Mwanariadha wa Kenya Brigid Kosgei, ameandikisha rekodi mpya ya dunia katika mbio za Marathon, akiwa na umri mdogo wa miaka 25. Kosgei alivunja rekodi ya dunia ya wanawake ya Paula Radcliffe ya saa 2:15:25 iliyokuwa imedumu tangu mwaka 2003.

Brigid Kosgei avunja rekodi ya mbio za dunia za wanawake Oktoba 13, 2019 Chicago.
Brigid Kosgei avunja rekodi ya mbio za dunia za wanawake Oktoba 13, 2019 Chicago. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Kosgei alishinda Chichago Marathon kwa upande wanawake, mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuweka muda wa saa mbili, dakika 14 na sekunde nne.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25, mwezi Aprili, pia alishinda London Marathon .

Alivunja rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Mwingereza Paula Radcliffe' aliyoiweka miaka 16, ya saa mbili, sakika 15 na sekunde 15.

Kosgei alinyakua taji lake la pili mfululizo la Chicago kwa saa 2:14:04 katika mbio hizi zilizovutia watkimbiaji 45,000.

Mkimbiaji huyu mwenye umri wa miaka 25 aliongoza mbio hizi kutoka mwanzo hadi utepeni.

Alivunja pia rekodi ya dunia ya wanawake pekee ya saa 2:17:01 ambayo Mkenya mwenzake Mary Keitany aliweka jijini London mwaka 2017.

Alifuta rekodi ya Chicago Marathon ya wanawake ya saa 2:17:18 ambayo Radcliffe aliweka mwaka 2002.

Naye Cherono alimaliza ukame wa Kenya wa miaka miwili bila taji la wanaume la Chicago alipobeba taji kwa saa 2:05:45.

Alimaliza sekunde moja mbele ya raia wa Ethiopia, Dejene Debela naye Asefa Mengstu akafunga msururu wa tatu-bora (2:05:48).

Kosgei alifuatwa dakika sita baadaye na Waethiopia Ababel Yeshaneh (2:20:51) na Gelete Burka (2:20:55). Mwuingereza Radcliffe alitimka 2:15:25 katika London Marathon mwezi Aprili mwaka 2003.

Kosgei, ambaye alishinda London Marathon mwezi Aprili 2019 alikuwa ameapa kufuta rekodi ya Radcliffe mjini Chicago.

Mafanikio haya yanakuja, baada ya mwanariadha mwingine wa Kenya Eliud Kipchoge, kuweka historia kwa kumaliza Marathon ya umbali wa Kilomita 42.2 chini ya saa mbili, na kuwa mwanaridha wa kwanza duniani, kufanya hivyo.

Rekodi zote za mbio za Marathon duniani, Kilomita 42.2 na 21 sasa zipo mikononi mwa wanariadha wa Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.