Kipa wa Ufaransa kukosa msimu uliosalia wa ligi kuu ya Uingereza 2019/20
Kipa wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza Hugo Lloris atakosa msimu wote wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuumia kiwiko mwishoni mwa wiki iliyopita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Lloris alipata jeraha hilo wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Brighton ambao ulimalizika kwa Spurs kubandikwa mabao 3-0.
Golikipa huyo wa Ufaransa alishindwa kuokoa kikamilifu mpira wa mchezaji wa Brighton Pascal Gross katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Taarifa ya klabu hiyo hata hivyo inasema mchezaji huyo hatahitaji kufanyiwa upasuaji na kueleza kwamba mchezaji huyo ataonekana tena uwanjani msimu ujao.
Lloris amekuwa kwenye kiwango cha juu tangu alipojiunga na klabu hiyo na mwaka 2018 alikuwa kipa wa kwanza kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe la dunia katika fainali zilizofanyika nchini Urusi.
Spurs inasema mchezaji huyo anahitaji kupumzika na kufanuya mazoezi ya taratibu.