Maendeleo ya soka la vijana eneo la Afrika Mashariki
Timu ya taifa ya soka ya Uganda yenye wachezaji wenye umri chini ya miaka 15, wameibuka mabingwa wa taji la Afrika Mashariki na Kati baada ya kuilaza Kenya mabao 4-0 jijini Asmara nchini Eritrea.Haya yalikuwa ni mashindano ya kwanza kuandaliwa na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA. Tunajadili mafanikio ya mashindano haya.