Pata taarifa kuu
AFCON 2019-KEYA-TANZANIA

Kenya na Tanzania kufia uwanjani, mechi muhimu ya AFCON

Timu za taifa za Kenya na Tanzania zitachuana Alhamisi usiku katika mechi muhimu ya mchezo wa soka, kuwania taji la bara Afrika, michuano inayoendelea nchini Misri.

Wachezjai wa Harambee Stars wakifanya mazoezi kuelekea mechi muhimu dhidi ya Tanzania Juni 27 2019
Wachezjai wa Harambee Stars wakifanya mazoezi kuelekea mechi muhimu dhidi ya Tanzania Juni 27 2019 FKF
Matangazo ya kibiashara

Mataifa haya mawili yapo katika kundi C na mechi hiyo itachezwa kuanzia saa tano usiku saa za Afrika Mashariki katika wa uwanja wa June 30 jijini Cairo.

Harambee Stars inakwenda katika mechi hii ya pili baada ya kuanza vibaya, kwa kufungwa na Algeria mabao 2-0 sawa na Taifa Stars ambayo ilifungwa na Senegal pia mabao 2-0.

Hii ni mara ya kwanza kwa mataifa ya Afrika Mashariki kutoka ukanda wa CECAFA ndani ya miaka 43 kucheza katika michuano hii mikubwa barani Afrika.

Kuelekea katika mchuano huu mkubwa kati ya majirani hawa wawili, mashabiki wa kila upande wanaamini kuwa, timu yao itafanya vema katika mchuano huo ambao kila timu inahitaji kushinda ili kuwa na matumaini ya kufuzu katika hatua ya 16 bora.

Mshambuliaji wa Harambee Stars, Michael Olunga amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu lakini lengo letu ni kupata alama tatu muhimu.

“Tanzania ni jirani zetu, na mechi itakuwa ngumu sana,” alisema Olunga.

Kocha wa Tanzania Emmanuel Amunike, amesema mechi hii ni muhimu kwa Tanzania ambayo ilipoteza mechi ya kwanza.

“Mechi dhidi ya Kenya ni muhimu sana, ni lazima tushinde ili kufuzu katika hatua ya mwondoano,” amesema.

Kundi hili pia lina Algeria na Senegal ambazo zinapewa nafasi kubwa katika michuano hii.

Katika historia ya Tanzania katika michuano ya AFCON, haikuwahi kushinda mechi hata moja iliposhiriki mara ya mwisho nchini Nigeria, lakini ilipata ushindi wake wa kwanza mwaka 2004 wakati ilipoishinda Burkina Faso 3-0.

Historia kati ya nchi hizi mbili inaonesha kuwa, zimekutana mara 44. Kenya imeshinda mara 20, ikatoka sare mara 14 huku Tanzania ikishinda mara 14.

Ratiba ya Alhamisi, Juni 29 2019

Madagascar vs. Burundi
Senegal vs. Algeria
Kenya vs. Tanzania

Michuano nyingine ya AFCON kati ya nchi za Afrika Mashariki

Januari 12, 1968: 
Ethiopia 2-1 Uganda

Februari 6, 1970: 
Sudan 3-0 Ethiopia

Februari 29, 1976: 
Ethiopia 2-0 Uganda

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.