Pata taarifa kuu
UEFA-PLATINI-SOKA-FIFA-QATAR

Rais wa zamani wa UEFA Michel Platini akamatwa

Aliyekuwa rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini amekamatwa kuhojiwa kuhusu namna Qatar ilivyopata uwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2022.

Rais wa wa zamani wa UEFA Michel Platini
Rais wa wa zamani wa UEFA Michel Platini uefa
Matangazo ya kibiashara

Platini mwenye umri wa miaka 63, ambaye alichaguliwa kuongoza UEFA mwaka 2007, anashikiliwa na maafisa wa kupambana na ufisadi jijini Paris, kubaini kuhusu Qatar ilivyopata nafasi hiyo.

Raia huyo wa Ufaransa, aliongoza UEFA hadi mwaka 2015, kabla ya kufungiwa na na Shirikisho la sika duniani FIFA kwa miaka minne kwa kupokea Euro Milioni 1.8 kutoka kwa rais wa zamani Sepp Blatter.

Makala 22 yatakuwa mashindano ya kwanza ya kombe la dunia, kuandaliwa katika nchi ya kiarabu.

Hata hivyo, kumekuwa na madai kuwa Qatar ilishinda nafasi baada Kamati kuu ya FIFA kuhongwa.

Viongozi wa mashtaka nchini Uswisi nao wamekuwa wakichunguza madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.