Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Real Madrid ndio klabu yenye thamani kubwa zaidi Ulaya

media Wachezaji wa klabu ya Real Madrid REUTERS

Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania imeipiku Manchester United ya Uingereza kama timu yenye thamani kubwa zaidi barani Ulaya, ambapo ina utajiri wa paundi bilioni 3.22, imesema ripoti ya kampuni ya mahesabu na ukaguzi KPMG.

Ripoti hii ambayo imejikita katika mauzo ya biashara kwa mwaka wa fedha 2016-17 na 2017-18, ilitazama faida iliyotokana na matangazo mubashara, umaarufu, vifaa vya michezo na thamani ya uwanja.

Klabu za Tottenham na Liverpool ambazo zitacheza mchezo wa fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, zenyewe zinashika nafasi ya 7 na 9 kwenye orodha hiyo.

Klabu za Chelsea na Arsenal ambazo zitacheza mchezo wa fainali ya kombe la Europa League, zenyewe zinashika nafasi ya 6 na 8.

Manchester City yenyewe iko kwenye nafasi ya 5, hii ikimaanisha kuwa kuna jumla ya timu 6 za kutoka ligi kuu ya Uingereza katika jumla ya timu 10 zenye thamani.

Real Madrid ilishinda taji la klabu bingwa Ulaya kwa misimu miwili mfululizo ambapo takwimu hizi zilijumuisha, ikiongeza thamani yake kwa asilimia 10.

Klabu ya Scotland ya Celtic imo kwenye orodha ya timu 32 ikiwa ni timu ya kwanza kufanya hivyo.

Mkurugenzi wa KPMG, Andrea Sartori amesema kiujumla thamani ya vilabu vya Ulaya imeongezeka kwa asilimia 9 katika mwaka uliopita.

KPMG inasema kwa upande mwingine gharama za wafanyakazi zimeongezeka, ambapo gharama zao zimeongezeka kwa asilimia 4 na kufikia asilimia 63.

IFUATAYO NI ORODHA YA TIMU 10 ZENYE THAMANI ULAYA

Real Madrid - €3.224bn

Manchester United - €3.207bn

Bayern Munich - €2.696bn

Barcelona - €2.676bn

Manchester City - €2.460bn

Chelsea - €2.227bn

Liverpool - €2.095bn

Arsenal - €2.008bn

Tottenham - €1.697bn

Juventus - €1.548bn

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana