Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-FIFA

Mahakama Sierra Leone yafuta mashtaka ya rushwa dhidi ya rais wa chama cha soka Isha Johansen

Rais wa chama cha soka nchini Sierra Leone, Isha Johansen amefutiwa mashtaka yote ya rushwa dhidi yake na mahakama ya mjini Freetown.

Rais wa chama cha soka cha Sierra Leone, Isha Johansen
Rais wa chama cha soka cha Sierra Leone, Isha Johansen Crop FifaYoutube
Matangazo ya kibiashara

Kufutiwa mashtaka kwa Johansen sambamba na katibu mkuu wake Christopher Kamara, kunatoa nafasi ya nchi hiyo kuondolewa adhabu iliyokuwa imewekwa na shirikisho la kabumbu duniani Fifa.

Shirikisho la soka duniani Fifa liliifungia Sierra Leone mwezi October mwaka jana kutokana na Serikali kuingilia shughuli za mpira kwa kuwaondoa madarakani Johansen na wenzake.

Baada ya uamuzi wake, Fifa ilisema inasubiri kwanza kumalizika kwa kesi dhidi ya Johansen kabla ya kuchukua hatua nyingine ikiwemo kuondoa adhabu iliyowekewa.

Makataa ya Fifa yalitokana na hatua ya maofisa wa tume ya kupambana na rushwa nchini Sierra Leone kuwaweka kando Johansen na katibu mkuu Kamara na kulikabidhi shirikisho hilo kwa makamu wake wa rais Brima Mazola Kamara na naibu katibu mkuu Abdul Rahman Swarray.

Mashtaka ya awali dhidi ya Johansen na wenzake yalipunguzwa kutoka mashtaka 10 hadi 3.

Katika kipindi chote Johansen na Kamara wamekuwa wakisisitiza hawana hatia dhidin ya tuhuma zilizowekwa mbele yao.

Makataa ya Fifa kwa nchi ya Sierra Leone yalisababisha nchi hiyo kukosa nafasi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya nchini Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.