Pata taarifa kuu
AFCON-CAMEROON-GUINEA-CAF

Cameroon yatwaa taji la Afrika kwa vijana chini ya miaka 17

Cameroon imeshinda taji lake la pili katika mashindano ya vijana wasiozidi miaka 17, baada ya kuilaza Guinea katika mchuano wa fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon wakishangilia baada ya kushinda taji la Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, tarehe 28 April 2019
Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon wakishangilia baada ya kushinda taji la Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, tarehe 28 April 2019 www.cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Les Lions Indomitables, ilishinda mechi hiyo baada ya kupata mikwaju ya penalti 5-3, baada ya mchuano huo kumalizika kwa kutofungana.

Mara ya kwanza Cameroon kushinda taji hilo, ilikuwa mwaka 2003, wakati huo, mashindano haya yalifanyika nchini Swaziland.

Pamoja na kushinda taji hili, Cameroon itaongoza wawakilishi wengine wa Afrika, Guinea, Angola na Nigeria kwenda kutafuta ubingwa wa dunia nchini Brazil mwezi Oktoba.

Mataifa mengine ambayo yamewahi kushinda taji hili la vijana ni pamoja na Ghana mara mbili mwaka 1995, 1999.

Nigeria pia imeshinda mara mbili, sawa na Gambia pamoja na Mali iliyoshinda mwaka 2015 na 2017.

Burkina Faso, Ivory Coast na Misri imeshinda mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.