KENYA-LONDON MARATHON-IAAF
Brigit Kosgei anyakua medali ya dhahabu kwa upande wa wanawake, mbio za London Marathon
Brigit Kosgei ameshinda mbio za London Marathon kwa upande wa wanawake.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kosgei mshindi wa mbio za Chicago Marathon miezi sita iliyopita amemshinda bingwa mtetezi wa mbio hizo Vivian Cheruiyoit akitumia muda wa saa 2:18:20.
Amemshinda bingwa mtetezi wa mbio hizo na mkenya mwenzake, Vivian Cheruiyot aliyeshika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa saa 2: 20:14 huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na raia wa Ethiopia Roza Dereje aliyetumia muda wa saa 2: 20:51.
Mbio za Londomn Marathon ni mojawapo ya mashindano makubwa katika mchezo wa riadha duniani na hufanyika kila mwaka na washindi kujizolea medali na zawadi za fedha.