Pata taarifa kuu
AFCON-AFRIKA-SOKA-CAMEROON-GUINEA

Guinea na Cameroon kucheza fainali ya vijana barani Afrika

Guinea na Cameroon, zitamenyana katika fainali ya kutafuta taji la vijana wasiozidi umri wa miaka 17 barani Afrika.

Wachezaji wa Guinea wakisherehekea baada ya kufuzu hatua ya fainali April 24 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania
Wachezaji wa Guinea wakisherehekea baada ya kufuzu hatua ya fainali April 24 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Fainali hiyo itachezwa siku ya Jumapili, katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Guinea ilikuwa ya kwanza ya kufuzu baada kuifunga Nigeria mabao 10-9 kupitia mikwaju ya penalti, baada ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya 0-0 katika muda wa kawaida.

Mambo yalikuwa vivyo hivyo kwa Cameroon, ambayo waliwashinda Angola mabao 5-4 pia kupitia mikwaju ya Penalti.

Nigeria na Angola nazo, zitamenyana katika mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu, siku ya Jumamosi.

Licha ya kufika katika hatua hiyo, timu hizo nne zimefuzu kucheza fainali ya kombe la dunia kwa vijana nchini Brazil mwezi Oktoba.

Mwaka 2017 wakati michuano hii ilipofanyika nchini Gabon, Guinea ilifika katika hatua ya nusu fainali, na kumaliza nafasi ya tatu.

Cameroon nao, walifika katika hatua ya makundi mwaka 2017.

Guinea haijawahi kushinda taji hili lakini mbali na mwaka 2017, mwaka 2015 na 1995 walimaliza katika nafasi hiyo.

Hata hivyo, Cameroon watakuwa wanatafuta taji la pili, baada ya kushinda mwaka 2003, wakati fainali hiyo ilipofanyika nchini Swaziland, siku hizi inaitwa Eswatini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.